Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini watakiwa kuingilia kati ukatili dhidi ya watoto

82468 Dini+pic Viongozi wa dini watakiwa kuingilia kati ukatili dhidi ya watoto

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi wa dini nchini Tanzania wametakiwa kukemea vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili kundi hilo liwe katika mazingira salama.

Wito huo umetolewa leo Alhamisi Oktoba 31, 2019 katika mjadala uliowakutanisha viongozi wa dini, vijana na walimu uliolenga kupitia mkataba wa kimataifa wa haki za watoto.

Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa na naibu mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (Unicef), Francis Odhiambo zaidi ya asilimia 70 ya watoto nchini hukutana na vitendo vya ukatili.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti dhidi ya vitendo vya ukatili kwa watoto uliofanywa mwaka 2011.

Amesema asilimia 72 ya watoto wa kike hukutana na vitendo hivyo wakati kwa upande wa watoto wa kiume ni asilimia 71.

Ameeleza kuwa kwa kiasi kikubwa vitendo hivyo hufanywa na watu wa karibu lakini  watoto wamekuwa wakivumilia kwa  usalama wao. Kufuatia hilo vijana na wawakilishi wa watoto walioshiriki mjadala huo waliwaomba viongozi wa dini kuzungumza na waumini wao kuhusu athari za vitendo hivyo ili wabadilike.

“Tuna imani kwamba viongozi wa dini wana nguvu kubwa kwenye jamii, wanaaminiwa na kusikilizwa, tunaomba mtusaidie kupaza sauti kuhusu suala hili watoto wana wakati mgumu.”

“Mtoto akipitia ukatili atakuwa na picha hiyo na kama jamii itakuwa kimya ataona ni vitu vya kawaida, jambo ambalo tunapaswa kuliondoa kwenye jamii yetu,” amesema Rose Mweleko.

Baada ya mjadala huo viongozi wa dini kwa pamoja walitoa azimio la pamoja kushiriki katika kukuza, kulinda na kutambua haki za watoto.

Chanzo: mwananchi.co.tz