Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini wataja mambo manne ibada ya Krismasi

33453 Pic+viongozi Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar/mikoani. Viongozi wa dini wametilia mkazo mambo manne katika mahubiri ya Sikukuu ya Krismasi iliyosherehekea jana ya-kiwamo amani, kusameheana na viongozi serikalini kuombewa ili watende yaliyo mema huku wakionya kuhusu ongezeko la utoaji mimba, talaka.

Amani

Katika mahubiri yake jana, Kasisi msaidizi wa Kanisa Kuu la Anglikana la mtakatifu Albano, Dar es Salaam, Padri Meshack Malilo alisema hakuna Taifa lolote linaloweza kudumisha amani bila kuona haki ikitendeka kwa wanan-chi.

Alisema ni lazima haki ionekane imetendeka na ndio amani inaweza kutawala mahali popote huku akisisitiza kila mmoja kutekeleza wajibu wake kuanzia ngazi ya familia hadi katika jamii.

Katika mahubiri yake, Askofu wa Jimbo la Bunda na msimamizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Renatus Mkwande aliwataka Watanzania kuliombea Taifa na viongozi wake ili wadumishe Amani.

“Inawezekana kuna makosa yanafanyika maana hakuna binadamu aliyekamilika. Tuwaombee viongozi wa Serikali na siasa watende kazi yao vyema kama walivyokabidhiwa mamlaka hiyo.”

Akihubiri katika mkesha wa Krismasi, Padri wa Kanisa la Anglikana la St Alban, Meshack Maliro aliwataka Watanzania kutenda haki kuanzia ngazi ya familia hadi maeneo ya kazi ili amani iendelee kutawala.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex Mala-susa akihubiri katika Kanisa la Azania Front alisema, “Tutafakari juu ya amani yetu kama jamii. Amani ya kweli inaanzia ndani ya mtu mwenyewe. Mungu atujalie kila mmoja kulishika neno hili ili amani itawale.”

Katika Kanisa la Mtakatifu Peter, Askofu Msaidizi Jimbo Kuu Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa alisema, “Mungu uwaongoze vizuri viongozi wetu wa kanisa na Serikali ili waweze kuitunza na kudumisha amani ya hapa duniani.”

Kiongozi wa Kanisa la Inuka Uangaze, Boniface Mwamposa (Buldoza) alisema Krismasi inawakumbusha wanadamu kusambaza upendo na Amani huku Paroko wa Ka-nisa la Bikira Maria wa Fatima, Parokia ya Mwanjelwa Mbeya, Padri Gabriel Mwakasita akihimiza waumini wake kudumisha umoja, uelewano, upendo na mshikamano.

Akihubiri katika katika Kanisa la la Arusha International Baptist, mchungaji kiongozi, Profesa Harison Olang alisema ujumbe wa amani ndio mkubwa katika maadhimi-sho ya Krismasi.

Viongozi kuombewa

Paroko wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Padri Valentine Kavalo alisema wapo viongozi wa Serikali wasiothamini dini hivyo wanatakiwa kuombewa na kuwa na moyo wa huruma na kusamehe, “Tuombee amani maana kuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka kesho.”

Askofu mstaafu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Glorius Shoo alisema wapo waliopewa madaraka lakini wanayatumia vibaya kuwanyanyasa na kuwaonea wengine.

Askofu huyo ambaye sasa ni mchungaji kiongozi wa Kani-sa la Kilimanjaro International Christian Center (KICC) la mjini Moshi alisema, “Siku hizi baadhi yetu badala ya kumtukuza Mungu tumewatukuza wanadamu. Kunafanyika maonyesho ya fedha, ufahari na karamu za ulevi na ulafi. Mungu hatukuzwi.”

Mkuu wa KKKT, Dk Frederick Shoo aliwataka wenye uwezo na mamlaka kuwatendea haki wanyonge ili kuepuka kujitukuza na kujinufaisha binafsi.

Akihubiri katika ibada ya Krismasi, iliyofanyika katika Ush-arika wa Moshi mjini, Dk Shoo alisema,

Msaidizi wa askofu wa KKKT, Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Osca Lema alisema wapo watu wana-weka vinyongo dhidi ya watu wengine jambo ambalo pia huwafanya washindwe kuona hata fursa za maendeleo hivyo kusisitiza kusameheana.

Talaka

Kuhusu talaka, Dk Malasusa alisema ikilinganishwa na mi-aka ya nyuma, talaka zinazidi kuongezeka nchini na wanandoa wengi wanaishi kwa hofu.

“Siku hizi talaka zimezidi, jamii haina upendo wala hofu ya Mungu, hofu imejaa katika ulimwengu wengi waliopo kati-ka ndoa hawana hakika kama wataendelea kwa kuhofu,” alisema.

Askofu wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Jacob Ole Mameo alisema watoto wa mitaani wameongezeka kutoka-na na wazazi kutotimiza majukumu yao na ndoa kuvunjika, hivyo watoto kulelewa mazazi mmoja.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe alisema dhambi mifarakano katika familia imesababisha watu kutengana na kusababisha watoto kuteseka.



Chanzo: mwananchi.co.tz