Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini washauri jinsi ya kuibadili jamii

Wed, 6 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi wa dini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha waumini wao kuhusu afya na usafi wa mazingira ili kujiondoa kwenye hatari ya kupata maradhi.

Wito huo umetolewa leo Jumatatu Machi 4, 2019 na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) la kuhudumia watoto, Unicef, kupitia programu ya Maji, Usafi wa Mazingira na Afya (Wash).

Akizungumza wakati wa mkutano uliozikutanisha taasisi za dini, mkuu wa programu hiyo Francis Odhiambo amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuibadilisha jamii.

Amesema ajenda ya afya na usafi wa mazingira inapaswa kubebwa kwa ukubwa wake na kufanyiwa kazi na kila mmoja kwenye jamii.

“Tumeona hawa viongozi wa dini wapo karibu zaidi na waumini wao hivyo wanaweza kufanya kitu kuhamasisha suala la afya na usafi.”

“Watu wengi wanaugua na watoto wanapoteza maisha kwa sababu ya magonjwa yanayotokana na uchafu kwa pamoja tukiamua tunaweza kulimaliza tatizo hili,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz