Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini wahimizwa kuelimisha jamii kuhusu chanjo

41625e8c4fd80278ec0a87b15624dc5f Viongozi wa dini wahimizwa kuelimisha jamii kuhusu chanjo

Tue, 13 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MENEJA Mpango wa Taifa wa Chanjo, Wizara ya Afya Maendeleo, Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Dk Dafrossa Lyimo, amewaomba viongozi wa dini kusaidia kuelimisha jamii umuhimu wa kupata chanjo zote kwa ajili ya kuzuia magonjwa yanayozuilika.

Dk Lyimo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini wa mkoa wa Dodoma.

Alisema hayo kwenye warsha ya kusaidia kuelimisha waumini wao umuhimu wa kupata chanjo ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa yanayozuilika.

Aliwaomba viongozi hao wa dini, kukanusha upotoshaji unaojitokeza kuhusu chanjo hizo zinazotolewa kuwa zina madhara kwa wanaopatiwa. Alisema kuwa hofu iliyojengeka kuwa huduma hiyo kiafya siyo nzuri, ni taarifa za uzushi.

Akizungumza na viongozi hao wa dini wakiwemo mashehe, maaskofu, maimamu na wachungaji, alisema kutokana na wao kuwa karibu na waumini, serikali kupitia wizara husika wana imani elimu hiyo itawafikia kwa wakati na uhakika, ukizingatiwa kuwa wanaaminiwa.

“Nafasi mnazokuwa nazo za kila siku kukutana na waumini kupitia mikutano ya mihadhara, semina, makongamano na mtu mmoja mmoja, ni imani yetu sisi watumishi wa wizara ya afya elimu hii itawafikia na wataweza kushiriki kikamilifu kwenye kupatiwa huduma ya chanjo,” alisema.

Awali akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Ahmad Makuwani alisema mpango wa kudhibiti magonjwa yanayotibika kwa huduma ya chanjo, unaridhisha kutokana na mafanikio yanayoonekana kwa kiasi kikubwa hapa nchini.

Alisema mafanikio hayo yametokana na watumishi wa afya kuwafikia jamii kwenye maneo yao kwa wakati, ikiwemo utoaji wa elimu ya uhamasishaji wa umuhimu wa kupata chanjo kwa kila mtu mmoja mmoja ili wajikinge na maambukizi ya magonjwa yanayozuilika.

Dk Makuwani alitaja baadhi ya magonjwa yaliyodhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutibiwa na chanjo ni surua, polio, pepopunda na kifaduro, ambayo kwa hivi sasa hapa nchini imefanikiwa kupungua kwa kiasi kikubwa.

Aliwataka viongozi hao wa dini, kutambua kuwa bado kuna changamoto ya chanjo, ambayo imekuwa ikichechemea katika kupata matibabu yake, kama vile ya magonjwa ya surua na saratani ya uzazi kwa ajili ya mabinti haijawafikia kwa ubora zaidi.

Chanzo: habarileo.co.tz