Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini wahimiza uzalendo

82015 Pic+dini Viongozi wa dini wahimiza uzalendo

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi wa dini mbalimbali wamekutana leo katika kongamano maalum lililoandaliwa kuelekea uchaguzi, uchumi wa viwanda, amani, mahusiano, uzalendo na ustawi wa Taifa.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amesema kongamano hilo ni muhimu kwa sababu linazungumzia masuala ya uzalendo kwa mustakabali wa taifa.

Amesema viongozi wa dini wana kila sababu ya kukutana ili kujadili masuala mbalimbali ndani ya taifa lao hasa amani na uzalendo.

Mufti Zubeir amesema uzalendo ni nembo mojawapo inayomuonyesha mtu kwamba yeye ni mfuasi wa dini.

 “Kongamano hili lisiwe mwisho na isiwe lazima kufanyika Dar es Salaam, lizunguke kwenye kanda na miji mbalimbali kwa faida ya Watanzania wote,” amesema Mufti Zubeir.

Awali, Askofu wa Kanisa la Mito ya Baraka, Dk Bruno Mwakibolwa alisema ni jambo jema viongozi hao kukutana pamoja kwa umoja.

Pia Soma

Advertisement
“Vitabu vyetu vya dini vinatuagiza ndugu kukutana pamoja na leo tumekutana kwa umoja,” amesema Dk Mwakibolwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz