Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini wahimiza Magufuli kuendelea kuombewa

Fbfe575642aecd5cc8318c08b0fdde9c.jpeg Viongozi wa dini wahimiza Magufuli kuendelea kuombewa

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VIONGOZI wa madhehebu ya dini mkoani Manyara wamehimizwa kuendelea kumuombea Rais Joseph Magufuli katika kipindi hiki cha maombolezo ya siku 21 kwa vyombo vya kudumisha amani ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutuma salamu zake za rambirambi kwa Rais mpya Samia Suluhu Hassan na watanzania wote alisema viongozi hao wa dini wana nafasi kubwa ya kutoa mafundisho kwa waumini wao ya kuwafanya watanzania wote wanakuwa wamoja zaidi na si vinginevyo.

“Ni muhimu Watanzania wakadumisha amani na mshikamano kwa nchi katika kuenzi mazuri ya Rais wetu, viongozi wa dini ndio dira ya kufikia katika azma hiyo,” alisema.

Kwa mujibu Mkirikiti wakati viongozi wa dini wakiendelea kuwafundisha waumini wao kuacha maovu pia aliwaasa vijana kuacha kupokea taarifa zisizo rasmi na kuzisambaza kwa wengine kwani jukumu la kutoa taarifa ni la vyombo na mamlaka husika za serikali.

Mkirikiti aliwataka wana Manyara kutumia siku za maombelezo ya kitaifa kuenzi matendo yake kwa vitendo na kuhimiza kuwa wamoja.

“Watumishi wa serikali kila mtu katika nafasi yake ni muda muafaka wa kuendelea kutoa huduma stahiki kwa wananchi huduma za afya, umeme, maji na kuacha kuwanyanyasa wananchi kwa kuwa Mheshimiwa Rais alitetea haki za wananchi wanyonge,” alisema.

Mwandishi wa habari wa kituo cha Clouds Media Group, Yusuf Daiy mkoani hapa alisema kwa wanahabari wamepata pengo kubwa kwani katika hotuba zake mbalimbali alikiri utendaji kazi wa vyombo vya habari na namna vilivyo na mchango kwa taifa hili.

Kwa upande wake mwandishi wa habari kutoka kituo cha Wasafi Media TV Elias Ernest alisema Rais Magufuli alikuwa bado anahitajika kuboresha tasnia ya habari kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari aliyoipitisha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz