Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini toka nchi 17 wazungumzia amani Z’bar

32388 Pic+dini Papa Francis

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Mwaka jana Oktoba 18, Papa Francis akiwahutubia wajumbe wa mkutano wa kimataifa uliozungumzia ‘Dini kwa ajili ya amani’ alisema:

“Watu wote wenye mapenzi mema na hasa wale walioko kwenye nafasi za uongozi wanapaswa kuwa ni vyombo na mashuhuda wa ujenzi wa Injili ya amani, kwa akili, nyoyo na mikono yao. Hii inatokana na ukweli kwamba, amani ni sanaa inayopaswa kutengenezwa na kudumishwa na wote.”

Maneno ya Papa Francis ni kielelezo namna watu sehemu mbalimbali duniani waliyochoshwa na vita, migogoro inayoendelea kupandikiza mbegu ya chuki na uhasama.

Migogoro inayoendelea duniani vikiwamo vita visivyo fika mwisho, mivutano ya kisiasa na matatizo ya kiuchumi umewafanya viongozi wa dini zote za Kiislamu na Kikristu kufanya mikutano ya kukumbushana umuhimu wa amani na maendeleo kwa jamii.

Hivi karibuni viongozi wa dini hasa za Kiislamu na Kikristu kutoka nchi 17 walikutana Visiwani Zanzibar kuzungumzia migogoro ya kisiasa na machafuko yanayoendelea duniani na namna ya kushirikiana katika kuhubiri amani kwenye nyumba zao za ibada.

Dk Alex Gehaz Malasa ambaye ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, akichangia mjadala anasema:

“Lazima tusambaze upendo kama Mungu alivyotutaka ili jamii ibaki kuwa na amani kuliko machafuko.”

Anasema dunia imeharibika kwa sasa wananchi wanatenda matendo yalio kinyume na mafundisho ya dini zao, jambo ambalo halipaswi kunyamaziwa kwa sasa.

Naye Padri George Jacob kutoka Nigeria anasema lazima dunia iamke na kuleta umoja kwa walimwengu wote kinyume chake jamii itazidi kuelekea kubaya.

Anasema machafuko yanayoendelea kumwaga damu za wasiokua na hatia yanatokana na binadamu kukataa mafundisho ya vitabu vitakatifu ambavyo vimekemea mapigano na machafuko kwa wanadamu.

Mshiriki kutoka Italia, Florentine Mallya anasema kutokana na yanayoendelea duniani kuna umuhimu wa kuhubiri upendo na amani.

Mallya ambaye ni padri wa Kanisa Katoliki nchini humo anasema licha ya wao kuhubiri amani na upendo cha kushangaza wapo baadhi ya watu wamekua wakivuruga amani na utulivu.

Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga ambaye alikuwa miongoni mwa wenyeji wa mkutano huo aliwataka waumini wa dini zote duniani kufuata na kutii taratibu za dini zao ikiwamo kuacha kukwaruzana kutokana na tofauti za kiimani.

Anasema kwa miaka mingi tangu enzi za mitume kumekuwapo na tofauti za kimani, lakini hakukuwahi kuwa na malumbano baina ya pande hizo za dini badala yake watu wote waliishi kwenye umoja na mshikamano ambao hivi sasa amesema umeanza kupotea. ‘’Hata kiongozi wa dini yetu Mtume Muhammad (S.A.W) hakuwahi kuwatenga wala kutofautiana na wasiokua Waislamu, hivyo si vyema waumini kufanya yasiopendezwa na Mungu.



Chanzo: mwananchi.co.tz