Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini mkoani Kigoma wazungumzia amani, haki

86245 Amani+pic Viongozi wa dini mkoani Kigoma wazungumzia amani, haki

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Kigoma wamewahimiza viongozi wenzao nchini kuhubiri  amani na kusema ukweli linapofanyika jambo lisilo sahihi katika jamii.

Wametoa kauli hizo leo Jumatano Novemba 27, 2019 katika kongamano la viongozi wa dini kujadili  unyanyasaji wa kijinsia na afya ya uzazi.

Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Iddi Kiburwa amewataka viongozi wa dini mkoani humo kuwa sauti ya wanyonge ili waweze kupata haki zao.

"Unyanyasaji wa aina yoyote katika jamii ni jambo baya na halikubaliki, viongozi wa dini tuna wajibu mkubwa wa kuwasemea wasiokuwa na sauti ili wapate haki kwani bila hivyo amani katika jamii inaweza kupotea na nchi kuingia katika vurugu," amesema Sheikh Kiburwa.

Amesema viongozi wa dini wana jukumu la kusimamia mambo mazuri yanapofanyika na kukemea maovu, kuwataka kuongozwa na maadili kupitia maandiko.

Padri wa Kanisa Katoliki Parikia ya Kigoma, Casius Rwegoshora amesema majukwaa ya dini yatumike kusambaza ujumbe kwa jamii,  kuhimiza haki na upendo.

Chanzo: mwananchi.co.tz