Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini Kibondo watoa hamasa waumini kupata chanjo ya Corona

Kig Viongozi wa dini Kibondo watoa hamasa waumini kupata chanjo ya Corona

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

Jitihada za viongozi wa dini kuhimiza waumini wao kuchanja zimekuwa zikifanyika katika nyumba za ibada licha ya mitazamo mbalimbali na upotoshaji ambao umekuwa ukiendelea katika mitandao ya kjamii.

Wamesema iliwapasa kuchanja ili kuwa mfano kwa waumini ambao walikuwa wametandwa na hofu na maswali mengi juu ya chanjo hiyo, ila kutokana na hamasa hiyo hofu na mitazamo vimeondoka na sasa muitikio ni mkubwa wa waumini kujitokeza kuchanja ili kuepukana na madhara yatokanayo na ugonjwa.

Askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Kibondo, Sospita Ndenza, amesema mwanzilishi wa kulinda afya ni Mungu mwenyewe ndio maana mitume na manabii wote walikuwa wanaponya afya za watu kwa ajili ya kuboresha afya na kuwa tukimuheshimu Mungu tutaziheshimu pia mamlaka zilizowekwa duniani.

“Wanaopinga tuwapuuze kwakuwa hawana elimu ya kutosha juu ya chanjo, tusikilize maelekezo sahihi ya serikali yetu ambayo haipo tayari kuona mtanazania akipoteza uhai, tukisema chanjo sio sahihi tutakuwa tunakosea kwakuwa sisi sio wataalamu wa eneo hilo,” ameeleza Ndenza.

Sheikh wa wilaya hiyo, Kassim Athuman, amesema hapaswi mtu kuacha kuchanja kwa kuwa atakuwa anajiingiza kwenye mauti ya mwili kwani maandiko yenyewe yanataka watu walinde afya zao na kwamba yamekataza watu waiingize nafsi zao katika maagamivu yanayopelekea kifo.

“Mimi nimechanja ili kuwa mfano kwa waumini kwani Mungu anataka kiongozi kuwa mfano, nawasishi waumini na jamii nzima kw aujumla kuacha mzaha kwa kusikiliza maeneno yenye upotoshaji na kuchagua kuchanja kwani chanjo zilikuwepo toka tunazaliwa na zitaendelea kuwepo,” amesema Athuman.

Muumini wa kikristo, Amina Sostenes, kutoka Biturana emesema kutokana na hamasa inayotolewa na serikali kupitia wahudumu wa afya pamoja na na viongozi wa dini, katika maeneo ya ibada amehamasika kuchanja na kuhimiza watu kutopuuzia hamasa hiyo, ili kujikinga na ugonjwa wa UVIKO -19 kama inavyosisitizwa na serikali.

Yusuph Said, kutoka Makondeko, amekiri jitihada za serikali kupambana na ugonjwa wa UVIKO -19 pamoja na mafundisho wanayoyapata kutoka kwa wataalamu wa afya na viongozi wa dini na hivyo kuaamua kuchanja.

“Sitaendelea kusikiliza maneno ya vijiweni maana kuna maneno mangi yanayojitokeza na mengi yao yakilenga kupotosha umma nawaomba wananchi wenzangu tuunge nguvu jitihada za serikali pamoja na gharama zinazotumika kwa kuchanja na kuwahamasiha wengine kuchanja,” amesema.

Chanzo: ippmedia.com