Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa dini Kanda ya Ziwa wataka mabaraza ya ardhi ya kata yapunguziwe nguvu

Viongozi Pic Viongozi wa dini Kanda ya Ziwa wataka mabaraza ya ardhi ya kata yapunguziwe nguvu

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Viongozi wa jukwaa la Kiimani wa Mikoa ya Kagera, Mwanza na Mara wamependekeza kurekebishwa kwa sheria za usimamizi wa Mabaraza ya Kata ya Ardhi ili yaiwe na uwezo wa kufanya uamuzi, badala yake yaishie kuwa chombo cha usuluhishi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 4, 2021 na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeeleza kuwa pendekezo hilo limesomwa Mwenyekiti Mwenza wa jukwa hilo, Sheikh Haruna Kichwabuta mbele ya Waziri William Lukuvi walipokutana Mjini Dodoma.

Sheikh Kichwabuta amesema baada ya kujadiliana, wamebainisha changamoto mbalimbali zinazosababishwa na mabaraza ya kata ya ardhi ambayo ni pamoja na miingiliano ya kimamlaka katika kufanya uamuzi, uelewa duni wa wajumbe kuhusu masuala ya kisheria, upendeleo, ukata, rushwa, siasa,

Askofu Abednego Keshomshahara wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania, Jimbo la Kaskazini Magharibi -Bukoba amesema wamelazimika kujadili changamoto hizo kwa kuwa hadi baraza la kata linasimamiwa na mamlaka tofauti hali inayosababishwa kutoeleweka nani msimamizi anayepaswa kuwajibika.

Akipokea taarifa ya mapendekezo ya jukwaa hilo, Waziri Lukuvi amesema Serikali inatambua changamoto hiyo na tayari muundo unaandaliwa utakaowawezesha wenyeviti wa mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya kuajiriwa kwa masharti ya kudumu mara baada ya kukamilika kwa miongozo na taratibu za Utumishi wa Umma.

Kwa mujibu wa Lukuvi, hatua hiyo inatokana na Bunge kufanya marekebisho ya sheria iliyokuwa inaelekeza wenyeviti hao kuajiriwa kwa mkataba wa miaka mitatu.

‘‘Marekebisho hayo yalifanyika ili kuondoa changamoto za mlundikano wa mashauri katika mabaraza ya ardhi wakati wa kusubiri mwenyekiti mwingine ateuliwe, hayo mambo ya rushwa yamejitokeza zaidi pale ambapo mwenyekiti hana uhakika wa kubaki katika nafasi yake mara muda wake unapokwisha,’’ amesema

Chanzo: mwananchidigital