Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Kikristu, Kiislamu nchini Tanzania kujadili uchumi wa taifa

Wed, 10 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakristu na Waislamu nchini Tanzania wameungana pamoja kutaka kujenga uchumi wa kitaifa kwa kuhamasisha mfumo wa soko jamii ambao utamnufaisha kila mmoja kutokana na shughuli anayofanya.

Ili kufikia lengo hilo, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Baraza la Wakristu Tanzania (CCT) wameandaa warsha ya siku mbili, Julai 10 na 11 itakayowakutanisha viongozi wa dini zaidi ya 100 kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili nao wakawafundishe waumini wao.

Akizungumzia warsha hiyo leo Julai 9, 2019  jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TEC, Padre Charles Kitima amesema jukumu la kuwajenga waumini kiroho ni la kwanza lakini sasa wameamua kuwajengea uwezo waumini haohao juu ya namna ya kunufaika na mfumo wa soko jamii badala ya kuwaacha watu wa nje wakinufaika na soko huria.

“Tunataka kuwajengea uwezo wananchi kumiliki uchumi wetu, tuna fursa kubwa kwenye ujasiriamali na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali lakini hatuzitumii. Nchi yetu imegeuka soko kwa bidhaa kutoka nchi nyingine, sasa tunataka tulitawale soko letu wenyewe kwa bidhaa zetu,” amesema.

Kiongozi huyo wa TEC amebainisha warsha hiyo ya viongozi wa dini itaambatana na uzinduzi wa kitabu cha Mfumo wa soko Jamii wa Tanzania (Social Market Economy Model for Tanzania) ambacho kimeandikwa baada ya wataalamu kufanya utafiti kwenye eneo hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz