Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana 50 kulipiwa mahari

Islam 51969 Vijana 50 kulipiwa mahari

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kiislamu ya Al- Hikma Foundation imetangaza kuwalipia mahari vijana 50 ambao wanahitaji kuoa.

Akizungumza katika mashindano ya 23 ya kimataifa ya uhifadhi wa Qur’an ambayo yamefanyika jana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Nurdin Kishki amesema kuwa mahari hiyo haitawahusu wale wanaotaka kuongeza mke wa pili.

Kishki amesema sharti hilo limewekwa kwa asiye na mke na sio lengo lake kusaidiwa wanaotaka kuongeza mke wapili.

“Tutafanya ndoa ya pamoja ya watu 50 mahari tutatoa Sisi Al-Hikma Foundation masharti usiwe unaongeza mke wa pili ndoa itafanyika Dar es salaam chini ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live