Taarifa ya Amri kutoka Vatican ilikataa na kupinga vikali juu ya kila kitu kuhusu Mahusiano na Ndoa za jinsia moja, pia Vatican ilitoa kauli na kusema kuwa Kanisa Katoriki halitabariki ndoa za jinsia moja kwani Mungu hawezi kubariki dhambi hata siku moja.
Amri hiyo na mapendekezo yalitolewa na Vatican tarehe 15 March 2021 na kuchapishwa na vyombo MbaliMbali vya habari Duniani Ili kujibu swali lililoulizwa kuhusu kama makasisi.
Viongozi wa ngazi za juu za dini ya kikatoriki (Maaskofu na Mapadre) wanaweza kubariki wanandoa wa jinsia moja, Shirika la Congregation for the Doctrine of the Faith (CDF), lilichapisha amri inayosema kwamba baraka kama hizo "haziwezi kuchukuliwa kuwa halali". Ambapo Jibu hili liliidhinishwa na Papa Francis na kuwa amri.
"Vatican inatambua, kuelewa uwepo wa ndoa na muunganiko kati ya Mume na Mke na sio vinginevyo, hivyo Muunganiko wa Jinsia moja Mwanaume na Mwanaume au Mwanamke na Mwanamke hautatambulika" - Vatican.
Papa Francis naye alikubali kupitisha Amri hiyo iliyotolewa na Vatican. Tarehe 25 January 2023, Papa alijitokeza na kusema kuwa Mahusiano Jinsia Moja ni Dhambi lakini sio Uhalifu, akasisitiza kwa kusema "Mungu anawapenda watoto wake wote" - ujumbe uliandikwa na Mtandao wa PBS-NEWS-HOUR.
Kulingana na mafundisho ya Kikatoliki, ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni sehemu ya mpango wa Mungu na inakusudiwa kwa uumbaji wa watoto.