Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Kwanini Wakristo wanasherehekea Krismasi na ilianza namna gani?

Video Archive
Mon, 10 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ninaitwa Mchungaji Christosila Petro Kalata kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Mbezi Beach.

Mada ya leo inaongozwa na swali kwa nini Wakristo wanasherehekea Krismasi na ilianza namna gani?

Krismasi ni tukio linalotokea ulimwenguni kote kila mwaka na ni moja ya sherehe za Wakristo wakijumuika na watu wengine duniani, hufanyika Desemba 25 kwa makanisa ya Magharibi.

Ulimwengu umegawanyika maeneo manne; Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi. Simulizi zinaelezea kulikuwa na sherehe za kipagani watu wa mashambani walikuwa na sikukuu zao za kuabudu jua ambapo lilikuwa likichomoza na kuleta miale wakiona ni kitu chenye nguvu na kuleta nuru ulimwengu na kwa tafsiri zao waliona ni kitu chenye nguvu ya ajabu katika maisha yao.

Sherehe hiyo ilikuwa inakaribiana na sikukuu ya kuadhimisha kukumbuka kuzaliwa kwa mwokozi Yesu Kristo, hivyo wataalamu wa maandiko wakaona kuwa upo uwezekano mkubwa wale waliokuwa wanamuabudu Mungu wa kweli ambaye ndiye aliyemtuma Yesu Kristo kuuvaa mwili wa mwanadamu.

Unajua Yesu Kristo alikuwa ni nafsi ya Mungu iliyozaliwa kupitia mwanadamu, waliona kwa nini siku hiyo ya wapagani isihuwishwe na siku ya Krismasi iwe chaguo sahihi la kumtukuza Mungu.

Ninaona ilikuwa ni hekima ya wale Wakristo wa mwanzo waliotumia njia ya kuwavuta hata wengine ambao walikuwa hawaelewi, hawamjui Mungu wa kweli, hawamjui Yesu Kristo aliyetumwa.

Basi kupitia sikukuu zao hizohizo wakaiweka sikukuu ya Krismasi haikuwa mbali na hiyo siku ya wapagani, kwa hiyo, Krismasi ikawa imeunganishwa na ile sherehe ilifanywa ikawa moja tu ya kukumbuka Mungu kuja katika ulimwengu huu kumuokoa mwanadamu aliyepotea kwa njia ya Yesu Kristo.

Unajua ni katika kufanya hivyo wale wasiomjua Mungu wa kweli wanaweza kuuona utukufu wa Bwana aliyeumba hilo jua. Wapo watu hadi hii leo hawana imani au amani na sikukuu hii ya Krismasi wakiamini imetiwa doa na ile sikukuu ya wapagani waliokuwa wanaabudu jua.

Lakini Wakristo kwa muda mrefu, nasema hivyo wameamini kuwa injili ni mbegu ambayo imepandwa mioyoni mwa watu na inapopandwa watu hawa wanamzalia Mungu matunda na kupatikana Wakristo wengi wapya ambao wanaingizwa kwenye kusanyiko la watoto wa Mungu, ndiyo maana idadi imekuwa ikiongezeka ni kwa njia ya mbegu ya injili, yaani habari njema.

Si hivyo tu, injili ni habari njema kwa watu wote na siyo kwamba inavuka mipaka ya tamaduni za watu kama tunavyosema pale kwamba, utamaduni ule wa wapagani kwa kutumia injili walionyeshwa kwamba kuna Mungu wa kweli ambaye ametumwa na Mungu yaani Yesu Kristo.

Pia inaleta mabadiliko kwa tamaduni ambazo ziko kinyume na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Ninaweka utangulizi huu wa kwa nini Wakristo wanasheherekea Krismasi. Wakristo hawasheherekei Krismasi kwamba ndiyo wakati ambao Yesu anazaliwa, bali wanakumbuka kazi njema ambayo imefanywa na Mungu katika ukombozi wa mwanadamu inafanana sana na kipindi kile ambacho wana wa Israel katika agano lile la kale walikuwa wametolewa na Mungu. Mungu amewaokoa kutoka utumwa wa kutumikishwa katika nchi za Misri, Babeli na nchi nyingine wakatawanyika huko na huko duniani.

Wao katika kipindi kile walikuwa wanamngoja Masiya yaani Yesu Kristo, hao ni wana wa Israel.

Kanisa leo tunasema Yesu Kristo analijia kanisa lake. Ndiyo maana Wakristo wanasherehekea ukombozi. Krismasi ni ukombozi, mtu aliyekombolewa anashangilia, aliyekombolewa anaimba Zaburi, aliyekombolewa anatumia nguvu za Mungu, miujiza ya Mungu katika kuleta mabadiliko katika mwili wa mwanadamu, roho na nafsi na ndiyo maana wanasherehekea.

Tutaendelea kuona katika makala nyingine zinazokuja hasa kwa nini tunasherehekea Krismasi.

Leo tumeona haya mapokeo jinsi ambavyo watu wale walikuwa wanasherehekea sikukuu hii kama nilivyosema Yesu Kristo ni habari njema kwa ulimwengu, habari njema kwa watu waliokosa tumaini, kwa watu ambao uchumi wao si mzuri analeta habari njema ya kufungua ufahamu wetu ili tutumie hekima na maarifa ambayo Mungu ametupa.

Katika kusherehekea kujikumbusha ni kuwa Mungu ametupa vipawa na karama nyingi. Huu ni mtaji wa ajabu kabisa ambao Mungu amempa mwanadamu hekima na akili, ni kumuweka Mungu namba moja na kumuweka kipaumbele cha kwanza kwa sababu anakupa akili ya kutumia vile ambavyo amekupa katika mazingira ambayo amekuweka.

Kuna watu mpaka leo hawaelewi vitu ambavyo vimewazunguka, wamezungukwa na utajiri mkubwa.

Itaendelea Jumapili ijayo



Chanzo: mwananchi.co.tz