Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO:Askofu wa Kanisa Katoliki asisitiza utunzaji wa amani, mazingira

Video Archive
Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam nchini Tanzania, Mhashamu Yuda Thadaeus Ruwa’ichi amewataka Watanzania kutambua kuwa amani iliyopo nchini ni zawadi na wana jukumu la kuendelea kuitunza.

Amesema zawadi hiyo inapaswa kwenda sawa na mihimili mingine ikiwemo haki, usawa na utekelezaji wa maendeleo yanayowagusa wote.

Akizungumza leo Jumatano Desemba 25, 2019 muda mfupi baada ya kumalizika kwa misa takatifu ya Krismasi iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Askofu Ruwa’ichi amesema kila mmoja anatakiwa kuhakikisha amani inaendelea kuwepo nchini.

“Namshuku Mungu kwa ajili ya zawadi ya amani ambayo ametupatia, niwakumbushe watanzania tuna jukumu la kutunza, kujenga na kushughulikia amani ili iendelee kuwepo,” amesema.

Pia amegusia suala la mabadiliko ya tabia nchi na kuwasisitiza Watanzania kutosahau utunzaji wa mazingira.

“Tuna changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi hivyo tunavyojipanga kuelekea kwenye maendeleo ni vyema tukaangalia pia suala la mazingira.”

“Tuna jukumu la kutunza mazingira ili na yenyewe yaendelee kututunza na kutuhifadhi sisi na vizazi vijavyo,” amesema Askofu Ruwa’ichi.

Chanzo: mwananchi.co.tz