Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upepo wa kisulisuli wavuta wengi Kanisa la Mlima wa Moto, vijana kibao wajitokeza

80983 Kisulisuli+pic Upepo wa kisulisuli wavuta wengi Kanisa la Mlima wa Moto, vijana kibao wajitokeza

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameendelea kufurika kwenye kanisa la Mlima wa Moto yanakofanyika maombezi maalum kwa ajili ya kuomba ndoa kwa wanaotamani kuingia kwenye taasisi hiyo.

Mwananchi limeshuhudia idadi kubwa ya waumini waliojitokeza kwenye ibada hiyo iliyopewa jina la ‘Upepo wa Kisulisuli.’

Mmoja wa wahudumu kanisani hapo ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake ameliambia Mwananchi leo Jumapili Oktoba 20, 2019 kuwa ibada ya leo imehudhuriwa na watu wengi kuliko ilivyo kawaida.

“Hili suala la upepo wa kisulisuli kwetu ni kawaida ila naona watu wametafsiri walivyoelewa wao, mwitikio ni mkubwa mno, sura nyingi naona mpya.”

“Kama mama alivyosema, leo yanafanyika maombi mazito kwa wanaohitaji ndoa, wale wenye haja kweli, watu wasifikiri wanaweza kuja kujipatia wanawake kwa urahisi hapa,” amesema mhudumu huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz