Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulinzi waimarishwa mazishi ya Askofu Chengula

29049 Askofu+pic TanzaniaWeb

Tue, 27 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Ulinzi umeimarishwa eneo ka Kanisa Katoliki Bikira Maria wa Fatma la Parokia ya Mwanjelwa Jijini Mbeya ambako inafanyikia misa ya kumuaga aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Mbeya, Evarist Chengula.

Watu wote wanaingia kanisani kwa utaratibu maalumu unaoambatana na ukaguzi wa askari waliosimama getini.

Watu wameanza kufika kanisani hapo leo Jumanne Novemba 27, 2018 saa 1:00 asubuhi na mwili wa Askofu Chengula umeingia kanisani saa 2:30 asubuhi.

Tayari viongozi wa Serikali na kisiasa wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila wamefika kanisani.

Viongozi wengine ni Naibu Spika, Dk Tulia Ackson,  Naibu Waziri wa Tamisemi, Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi maarufu 'Sugu' na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mbeya.

Endelea kufuatilia Mwananchi



Chanzo: mwananchi.co.tz