Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukraine washerehekea Krismasi kwa mara ya kwanza

Ukraine Washerehekea Krismasi Kwa Mara Ya Kwanza Ukraine washerehekea Krismasi kwa mara ya kwanza

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakristo wa Kanisa la Orthodoksi nchini Ukraine leo kwa mara ya kwanza wanasherehekea Krismasi mnamo Desemba 25.

Awali, Ukraine walikuwa wakitumia kalenda ya jadi ya 'Julian', ambayo pia hutumiwa na Urusi. Kwao Krismasi husherehekewa Januari 07.

Matumizi ya kalenda ya 'Gregorian' kama yalivyo mataifa mengi ya Magharibi ni muendelezo wa kuchukua hatua za kukinzana na taifa la Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alibadilisha sheria hiyo mwezi Julai, iliyowaruhusu raia wa Ukraine "kuachana na urithi wa Urusi" ikiwemo kusherehekea Krismasi mwezi Januari.

Katika ujumbe wa Krismasi uliotolewa Jumapili jioni, Zelensky amesema Waukraine wote sasa wapo pamoja.

“Sote tunasherehekea Krismasi pamoja. Katika tarehe hiyo hiyo, kama familia moja kubwa, kama taifa moja, kama nchi moja iliyoungana,” amesema Zelensky.

Katika jiji kuu la Kyiv, wenzi wa ndoa Lesia Shestakova, Mkatoliki, na Oleksandr Shestakov, ambaye ni Mwothodoksi, wanasherehekea Krismasi pamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live