Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukaaji wa mita moja kuepuka maambukizi ya corona watumika kanisani

Ukaaji wa mita moja kuepuka maambukizi ya corona watumika kanisani

Mon, 13 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sengerema. Waamini wa kikristo kote dunia leo wameazimisha sikukuu ya pasaka ambayo ni ukumbusho wa kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo huku wakiwa na tahadhari ya ugonjwa wa corona kwa kukaa mita moja wakiwa kanisani.

Katika parokia ya Yesu Kristu mfamle Sengerema mjini Jimbo la Geita waumini walikaa umbali wa mita moja kila mmoja kwa ajili ya kuepuka maambukizi ya ugonjwa corona ambao umetikisa dunia.

Misa hiyo iliongozwa na paroko wa parokia hiyo Patrick Hedrick ambaye amewataka waumini kufanya chaguo sahihi hapa duniani kwa kumjua Mungu na kutenda yaliyo mema ili kufika mbinguni.

Amesema kila mmoja atakwenda mbiguni kutoka kwenye kaburi lake alilozikwa hivyo matendo  mema yanatakiwa hapa duniani na kumtii Mungu.

Mmoja wa waumini waliohudhuria misa ya pasaka katika kanisa hilo Suzana Julias amesema hata wakiwa wanasali wanapaswa kuwa na tahadhari ya ugonjwa wa corona ambao umetikisa dunia na ndiyo maana leo wamekaa mita moja kwa kila muumini ili kuepuka maambukizi hayo.

Padri Hedrick pia amewakumbusha waumini kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa kutenda mema huku wakiwa nyumbani mwao kwa kuwa na tahadhari ya ugonjwa wa corona.

"Ndugu zangu tunatakiwa kusherehekea sikukuu ya pasaka hivyo tukae majumbani huku tukiwa na tahadhari ya corona inaua tunatakiwa kuwa makini."

Misa hiyo imedhuriwa na idadi ndogo ya waumini wengi wao wakisema ni tahadhari ya ugonjwa wa corona.

Chanzo: mwananchi.co.tz