Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujumbe wa Krismasi wa Mtume Mwamposa huu hapa

33414 Pic+mwamposa Mtume Boniface Mwamposa ‘Buldoza’

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtume Boniface Mwamposa ‘Buldoza’ wa Kanisa la Inuka Uangaze  amesema Sikukuu ya Krismasi ni siku inayowakumbusha wanadamu kusambaza upendo kila mahali.

Akihubiri katika ibada ya sikukuu hiyo katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam leo Jumanne Desemba 25, 2018, Mwamposa amesema Yesu alizaliwa duniani ili kuwaokoa waliogandamizwa na shetani.

"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, japo alizaliwa kwenye zizi la ng'ombe lakini hakuna aliyeweza kuifunika nyota yake kwani iliendelea kung'aa ndivyo ambavyo nyota yako itakuwa, hakuna atakayeifunika," amesema Mwamposa.

Amesema sikukuu hiyo inawakumbusha watu wakizaliwa pamoja naye, hata kama mtu atazungukwa na watu wabaya kiasi gani wema wake utamfunika na watashindwa kumfanyia ubaya.

Mwamposa aliwaombea waumini wa kanisa hilo kuvuka mwaka salama na kuanza mwaka 2019 kwa ushindi na mafanikio makubwa.

Amewaonya waumini hao kutosherehekea siku hiyo kwa kufanya dhambi ikiwamo ulevi badala yake waendelee kutenda mema.

"Unajua Yesu alipozaliwa mamajusi kutoka Mashariki ya mbali walikuja kumletea uvumba na manemane, nakuombea nawe pia ukutane na watu sahihi kwenye maisha yako watakaokuja kukuletea habari njema," amesema Mwamposa.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamesema siku ya Krismasi imekuwa njema kwao kwa sababu wamepata ujumbe unaogusa maisha yao.

"Naomba Mungu nivuke mwaka salama na haya mahubiri ya Mtume Mwamposa yafanyike baraka kwangu," amesema Anitha Hanaliya.



Chanzo: mwananchi.co.tz