Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutaendelea kuunga mkono Serikali- Askofu Niwemugizi

Baba Askofu (600 X 309) Askofu wa Jimbo la Rulenge Ngara Mhashamu Severine Niwemugizi

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu wa Jimbo la Rulenge Ngara Mhashamu Severine Niwemugizi amesema kuwa kanisa katoliki litaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Sita katika kuboresha kiwango Cha taaluma kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi, amebainisha hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu iliyofanyika katika shule ya sekondari Severine wilayani Biharamulo mkoani Kager akisisitiza ufundishaji wa nadhalia na vitendo ili kumjenga mwanafunzi katika misingi ya Uongozi bora

Askofu huyo amesema kuwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ni kwa sababu Kanisa hilo linapenda kuona taifa likiwa wataalamu wenye sifa zinazoendana na soko la ajira kimataifa na kikanda hasa ukanda wa Afrika wa Mshariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live