Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumia karama ya akili kufanikiwa 2019

34056 Mahubiri+pic Tanzania Web Photo

Mon, 31 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Naitwa Mchungaji Christosiler Kalata kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Beach, Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Ni siku njema ya Jumapili tunapouaga mwaka 2018 na kuingia mwaka 2019, nikutakie kila lenye heri mwaka mpya wenye mafanikio.

Ukisoma kitabu cha Mwanzo 28:4 neno la Mungu linasema “Akupe mbaraka wa Ibrahim, wewe na uzao wako pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, Mungu aliyompa Ibrahim.”

Baraka aliyopewa Ibrahim ni nchi, baraka aliyotupa Mungu sisi Watanzania ni nchi ya Tanzania.

Waumini wa Agano Jipya ni uzao wa Ibrahim, nasi tunashiriki Baraka hizi.

Wewe ambaye umeweka tumaini lako kwa Mungu, hakika tegemea kuwa na mwaka mpya wenye mafanikio na baraka tele kwa sababu hiyo ndiyo ahadi yake kwako.

Mungu ametupa hazina kubwa katika uumbaji wake, hazina hiyo ni akili.

Mungu anatudai karama hii tuitumie kikamilifu mwaka 2019, wakati tunajipanga kuingia mwaka mpya lazima ujizatiti kikamilifu katika mambo ya kiroho na kimwili hasa kiakili na kiuchumi.

Nayataja mambo haya kwa sababu mwanadamu aliyeumbwa na Mungu hana budi kupitia changamoto nyingi kwa msaada wa Mungu na anapovuka hufanyika barka.

Mwaka 2018 tumeona nchi ikipita katika misukosuko mingi ya kiroho, kiuchumi, kisiasa huku jamii ikiguswa katika eneo moja hadi jingine.

Swali ninalojiuliza ni hili, hivi wapo wasiotaka nchi hii kuwa na maendeleo? Na kama wapo wanatushambulia kwa njia zipi? Ni watu binafsi, taasisi, au nchi?

Mwaka 2019 ni mwaka wa kufahamu kuwa tunapotaka kuwa na uchumi mzuri ni mapambano pia ya kukua kiroho.

Katika kitabu cha 2Theselonike 3:2 neno la Mungu linasema, tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.

Wewe Mtanzania ambaye Mungu atakuvusha kuuanza mwaka mpya wa 2019 hupaswi kuwa mzururaji, bali unapaswa kufanya kazi kwa bidii ili ujiongezee kipato.

Ukifanya kazi kwa bidii utasaidia itakuwa rahisi kwako kupata mafanikio, na ukifanikiwa basi jamii inayokuzunguka pia itafanikiwa.

Wakristo tunayo imani, sisi tuna matumaini makubwa, tunataka kuvuka, lazima tuwe na msimamo wa kiroho.

Tumeona Rais Dkt John Magufuli, akibomoa misingi ambayo haikuwa rafiki kwa Watanzania, misingi ambayo imeitafuna nchi kwa muda mrefu, unaweza kujiuliza ujasiri alionao kiongozi huyu wa nchi anaupata wapi?

Ni kutoka kwa Mungu anajua nini afanye na kwa wakati gani!

Wakristo na Watanzania wote hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yale ambayo yamefanywa na kiongozi huyu.

Mtu yeyote anayeongozwa na Mungu kuwatoa watu katika umaskini lazima akutane na vita kubwa.

Mwaka mpya 2019, tumuombee Rais wetu Mungu amuongezee ujasiri!.

Watanzania na wote walioko katika taasisi mbalimbali wawe majasiri, wawe na uzalendo.

Tujenge nidhamu katika kazi, kwani tumesemwa sana sasa inatosha.

Mwaka mpya uwe wa mabadiliko makubwa, tukijenga mshikamano, tukigundua mbinu za adui, anazozitumia katika eneo la utamaduni, demokrasia, siasa, na hata katika masuala ya kijamii tutaweza kumshinda.

Hakuna ubaya wowote viongozi wa siasa kukutana na kiongozi wa nchi.

Kutokuzungumzia maendeleo ya watu na nchi ni kukosa uzalendo, viongozi wa dini wanaowajibu wa kukaa na Rais wao na kushauriana mambo ya nchi kwa sababu ni kitu ambacho kinampendeza Mungu.

Wenzetu katika nchi tunazosema zimeendelea, wao wanakaa pamoja na kuvumbua mbinu za kutunyonya, kutugombanisha.

Wanatutafutia kila aina ya mbinu, tukae muda mrefu bila kufanya kazi lakini wao wao wanaendelea kubuni kila aina ya bidhaa, na sisi kuendelea kuwa soko lao.

Mwaka mpya tuyajue hayo, tuwe na vya kwetu, tunao uwezo wa kutoka hapa tulipo na kupiga hatua itakayowashangaza wengi.

Jipange kuuanza mwaka ujao kwa mafanikio ili hata wale ambao walikuwa wanatubeza kuwa hatuwezi chochote washangae.

Heri ya mwaka mpya.



Chanzo: mwananchi.co.tz