Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tudarco yazindua shahada mpya ya uzamili

Wed, 18 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Chuo Kikuu Kishiriki  cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam (Tudarco) nchini Tanzania kimezindua shahada ya uzamili ya masuala ya Udiakonia.

Shahada hiyo itakuwa inatolewa katika mabara matatu ya Afrika, Ulaya na Asia.

Katika uzinduzi wa shahada hiyo uliyofanyika Tudarco jana Jumatatu Septemba 16,2019 ulihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwamo wanafunzi kutoka vyuo vishiriki vinavyofundisha kozi hiyo vya IDM kutoka Ujerumani, Silman ya Ufilipino na Stellenbosch cha Afrika ya Kusini.

Kozi hiyo ina lengo la kuandaa wataalamu watakaokwenda kuisaidia jamii katika masuala mbalimbali mathalani yenye uhitaji maalum wakiwemo walemavu, watoto, yatima na wanawake ili kuwatengenezea uwezo wa kujikwamua katika changamoto wanazokutana nazo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Hendrue Molel alisema kuzinduliwa kwa kozi hiyo itaongeza kozi ambazo wanazitoa chuoni hapo.

“Tumefurahi na kupokea kwa mikono miwili kozi hii kwa sababu ina manufaa makubwa sana kwetu kama taasisi na kama jamii ya Watanzania pia,” alisema

Pia Soma

Advertisement
Alisema wao kama taasisi wana wajibu wa  kuandaa wataalamu watakao toa huduma ya Udiakonia katika jamii pia ni fursa ya kuifikia na kutoa msaada kwa jamii inayotuzunguka.

Alisema kwa sasa wanaandaa mtalaa wa shahada ya kwanza itakayoitwa, shahada ya Udiakonia na huduma za kijamii (Bachelor of Arts and Diaconia Social Works).

Profesa huyo aliiomba jamii kufika ili kuwawezesha kupata utaratibu na vigezo vya kujiunga na kozi hiyo kwani ni fursa adhimu.

Naye  mratibu wa  Diakonia na Huduma za Jamii wa Tudarco, Dk Robert Charles alieleza kwa ufupi sifa za kujiunga katika shahada hiyo lazima uwe na shahada ya awali ambayo kwa Tanzania husimamiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Alisema kozi hiyo imesajiliwa nchini Ujerumani na  Tudarco itakuwa kituo cha mafunzo kama ilivyokuwa katika Vyuo Vikuu vya  Silman nchini Ufilipino, Jakata cha Indoneshia na Stellenbosch cha Afrika ya Kusini.

Chanzo: mwananchi.co.tz