Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tetemeko: Nilikaa chini ya kifusi kwa saa 52 nikisali Rozari

Basl Hbkok Maa Oldyh 1677141492 Nilikaa chini ya kifusi kwa saa 52 nikisali Rozari

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja raia wa Lebanoni, Bassel Habkouk, baba wa watoto wawili, alikuwa mmoja wa wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki ambapo zaidi ya watu 50,000 walipoteza maisha hivi karibuni.

Akisimulia kwa uchungu baada ya kumpoteza rafiki yake waliyekuwa pamoja, anasema alifikia kukata tamaa baada ya kuona wengine wakiokolewa lakini yeye aliyekuwa umbali wa mita 2 chini, hakufikiwa kwa haraka licha ya kufanikiwa kuwapa ishara waokoaji.



Bassel ambaye alikaa chini ya kifusi kwa saa 52 kabla ya kuokolewa, amesema katika sekunde 40 za kwanza, alimuita mama Bikira Maria hadi pale tetemeko lilipokoma, hakuwa ndani ya nyumba ila alifunikwa na kifusi cha majengo ya karibu.

"Nilipoanza kusali Rozari, nakili kupata nguvu na ushujaa kuwa nitaokolewa, nilishangaa kuzungukwa na hali ya ubaridi na hewa ya kutosha bila ya kujua imetoka wapi

"Mungu alinilinda na Mama Bikira Maria hakuniacha, sikupata kiu wala njaa, nalikuwa bado na hifadhi kidogo ya chakula," alisema Bassel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live