Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru kuchunguza matumizi ya Sh900 milioni Dodoma

49845 Pic+takukuru

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dodoma imesema inachunguza ufisadi wa Sh900 milioni katika miradi ya maji, ujenzi, elimu na afya.

Pia taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh152.3 milioni ambazo zingelipwa kwa wakandarasi ambao ufuatiliaji wa ukaguzi wa miradi ya maji umebaini hawakutimiza majukumu yao ipasavyo.

Akitoa taarifa ya kipindi cha miezi mitatu ya robo ya kwanza ya mwaka 2019 jijini Dodoma leo Jumatatu Aprili 1, 2019, Kamanda wa Takukuru mkoa wa Dodoma, Sostenes Kibwengo amesema taasisi hiyo ilifuatilia matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh9.8 bilioni.

Amesema lengo la kufuatilia miradi hiyo ni kujiridhisha iwapo fedha zinatumika vizuri, kwa wakati na iwapo inatekelezwa kwa ubora na thamani halisi ya fedha inapatikana.

“Miradi iliyofuatiliwa ni katika sekta ya maji, ujenzi, elimu na afya, katika miradi hiyo kiasi cha fedha Sh900 milioni zinachunguzwa baada ya viashiria vya jinai kuonekana,” amesema.

“Taasisi yetu inamtaka mkurugenzi wa kampuni ya Global Spec East Africa Limited ya Dar es salaam, Gaston Francis kuripoti mara moja katika ofisi za taasisi hiyo wilaya ya Mpwapwa (Dodoma),’’ amesema Kibwengo.



Chanzo: mwananchi.co.tz