Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TEC, CCT waahidi kumuunga mkono Rais Samia

7bd3f83bdbccfc6a7e4636239fef3d6d.jpeg TEC, CCT waahidi kumuunga mkono Rais Samia

Sat, 27 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAASKOFU wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), wameahidi kumuunga mkono na kushitrikiana kwa dhati na Rais wa Sita wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Samia aliyekuwa makamu wa Rais wa Tanzania, aliapishwa Machi 19, mwaka huu kuwa Rais wa Tanzania kutokana na kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John magufuli kilichotokea Machi 17, mwaka huu mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Rais akifariki duniani, makamu wa rais ataapishwa kuwa rais wa nchi kwa kipindi kilichosalia kabla ya uchaguzi mkuu unaofuata.

Wakitoa salamu za pole baada ya Misa Takatifu ya kumuombea pumziko jema Dk Magufuli, Makamu wa Rais wa TEC na Askofu wa Jimbo la Geita, Flavian Kassala na Mwenyekiti wa CCT, Dk Alinikisya Cheyo, walisema taasisi zao zinamhakikisha Rais Samia kuwa zitamuunga mkono na kumpa ushirikiano wa dhati katika uongozi wake kwa Watanzania.

“Sisi Maaskofu tunakuhakikishia Rais Samia sala na maombi katika kuongoza Taifa hili na tupo nyuma yako,” alisema Askofu Kassala na kuongeza kuwa, TEC wanamtambua Magufuli kuwa ni kiongozi aliyerejesha nidhamu ya utendaji kwa wananchi na kutamani maisha bora kwa kila Mtanzania huku akionesha imani thabiti kwa Mungu.

Akaongeza: “Magufuli anatukumbusha maisha ya duniani ni mafupi yasiyojulikana lini yatakoma na yeye alitumia muda wake kutekeleza mengi na kwa haraka. Mungu mwenye huruma atampokea kwake.”

Kwa upande wa CCT, Dk Cheyo alisema: “Sisi Wakristo wa Tanzania tunakuhakikishia tutakuunga mkono kwa hali na mali, umefanya mengi chini ya Rais Magufuli; hatuna mashaka na tutaendelea kushirikiana naye na kumuombea afya njema.”

Dk Cheyo alisema Rais Magufuli alikuwa shujaa aliyewaunganisha Watanzania bila kujali dini wala kabila jambo litakaloendelea kubaki mioyoni mwa Watanzania.

Chanzo: www.habarileo.co.tz