Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simulizi ya bibi na mjukuu walivyokufa kwenye ibada

94432 Bibi+pic Simulizi ya bibi na mjukuu walivyokufa kwenye ibada

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Tukio la kuaga miili ya watu 19 kati ya 20 jana liligubikwa na simanzi na vilio, huku simulizi za watu waliofariki zikiumiza mioyo ya watu hasa mtoto mdogo wa miaka minne aliyekufa na bibi yake.

Watu 20 walifariki dunia na 16 kujeruhiwa, Jumamosi iliyopita kufuatia mkanyagano uliotokea kwenye ibada ya Nabii na Mtume wa Kanisa la Inuka Uangaze, Boniface Mwamposa iliyofanyika katika katika Uwanja wa Majengo mjini Moshi.

Watu walikanyangana na kusababisha maafa hayo wakati wakigombea kukanyaga mafuta ya upako.

Vifo hivyo vilitokana na utelezi uliokuwa kwenye sehemu ya kukanyaga mafuta hayo, ambayo yailikuwa kwenye kasha lililofunikwa kwa plastiki ngumu na kusababisha watu wengi kuanguka na kukanyagwa na waumini wenzao.

Zoezi la kuaga miilli ya waliofariki katika tukio hilo lilikabiliwa na changamoto baada ya baadhi ya watu kushindwa kuaga miili hiyo kutokana na mvua zilizokuwa zinanyesha.

Miili hiyo iliwekwa katika viwanja vya Mashujaa mjini Moshi ambapo mamia ya watu walijitokeza kushuhudia tukio hilo la kuaga watu hao waliofariki dunia.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Hata hivyo mara baada ya zoezi hilo kusitishwa ndugu wa marehemu hao walitakiwa kuchukua miili ya wapendwa wao kwa ajili ya maziko huku vilio na simanzi vikitawala katika viwanja hivyo.

Mtoto aliyezua simanzi, Royality Shirima (4) alikuwa ameachwa na mama yake kwa bibi yake, lakini bibi huyo akaamua kwenda na mtoto huyo kwenye kongamano bila mama wa mtoto kujua.

Baba wa mama aliyefiwa na mwanae, Rashid Nsokolo, mkazi wa Kiboriloni, alisimulia kuwa binti yake alitoka asubuhi kwenda kazini na kumuacha mtoto kwa bibi yake, ambaye ni mwanafamilia pia.

Bibi huyo ilikuja kufahamika baadae alimchukua kwenda naye kwenye maombi.

Nsokolo alisema siku ya tukio yeye pamoja na binti yake walikuwa kazini na aliporudi jioni, alimuulizia mjukuu wake na kuambiwa alikuwa kwa bibi yake.

“Sisi tulienda kazini, na mtoto aliachwa chumbani kwa bibi yake ambaye alienda naye kwenye mkutano kwa Mwamposa na sisi hatukufahamu kama mtoto amepelekwa huko kwa kuwa ningezuia hilo.

“Baada ya muda kupita bila kumuona mjukuu niliuliza yuko wapi, nikaambiwa alilala kwa bibi yake, lakini asubuhi tulipoamka tulienda kwa bibi yake hatukuwakuta wote,” alisema.

“Ilinishtua ikanilazimu nipige simu polisi, ambapo niliambiwa kuna watu 20, wamefariki na wapo mochwari hospitali ya Mawenzi niende nikaangalie,” alieleza Rashid na kuongeza alimtuma mkewe kwenda hospitali kwenda kutambua maiti.

Alieleza mkewe alipofika chumba cha maiti aliutambua mwili wa mjukuu wake pamoja na bibi yake na walipewa taarifa kuwa walifariki kwa kukanyagana wakati wakigombea kukanyaga mafuta.

Mama wa mtoto aliyefariki, alishindwa kuzungumza kwani alionekana akilia kwa uchungu, akisema, “kwa nini Mungu umeruhusu haya, kwa nini Mungu umchukue mtoto wangu katika umri huu mdogo hivi.”

Chanzo: mwananchi.co.tz