Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sikukuu ya Eid El- Fitri: Mwezi kuandama Aprili 21 au 22

Sheikh Mruma G.jpeg Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Nuhu Mruma

Sun, 16 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Nuhu Mruma amesema Sikukuu ya Eid El-Fitri itakuwa kati ya Aprili 21 au 22 kutegemea mwandamo wa mwezi.

Mbali na hilo, Sheikh Mruma amesema sherehe za Eid El-Fitri kitaifa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam na swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, Bakwata makao makuu Kinondoni.

Sheikh Mruma ameeleza hayo Jumamosi Aprili 15, 2023 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mwenendo wa mwezi wa Ramadhani na uwezekano wa siku itakayosheherekea Sikukuu ya Eid.

“Swala itaanza saa moja na nusu asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika saa 8 mchana katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Itakayohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, (Sheikh Abubakar Zubeir) tunawatakia Waislamu na wananchi maandamizi mema ya sikukuu ya Eid,” amesema Sheikh Mruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live