Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheikh wa mkoa akemea wanaofuturisha bila kufuata misingi ya dini

60504 Futari+pic

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waislamu wametakiwa kuuheshimu Mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwamo kuzingatia ibada ya kufuturu na kufuturisha kama ilivyoelekezwa na Mtume (SAW).

Kauli hiyo imetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum alipofanya mahojiano maalumu na MCL Digital ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuwapo gumzo la watu kufuturisha bila kufuata misingi ya dini.

Alhad amesema kwa mujibu wa hadithi za Mtume Muhammad (SAW), kufuturu ni ibada, hivyo kucheza muziki au kufanya chochote kinachopingana na maagizo ya Mwenyezi Mungu ni kushusha hadhi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

"Kuushushia hadhi Mwezi huu ni kumchokoza Mwenyezi Mungu ambapo anaweza kuwapa kitu wasichokitarajia.  Hawa wasanii na wengine wote waache kumchokoza Mwenyezi Mungu kwa sababu adhabu yake hawaziweza, vita na yeye ni mbaya na huwa na madhara kwa anayeitafuta," amesema Alhad Salum.

Akifafanua kuhusu kufuturisha na kufuturu amesema kuwa kwa maelekezo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu  (RA) kufuturu ni kile kitu mtu anachokula mwanzo inapofika magharibi.

"Hadithi za Mtume (SAW) zimeelekeza kitu hicho ni tende au maji. Tende ni tunda lenye vitu vingi ikiwamo virutubisho kwa mwili na inarudisha sukari iliyopotea siku nzima wakati wa mfungo, lakini maji yanapatikana kula mahali" amesema.

Pia Soma

 

Kuhusu kufuturisha maskini

Amefafanua kuwa thawabu anazopata aliyefuturisha hazijalishi kufuturisha masikini au tajiri wote wanapata sawa.

"Kwa kuwa imeelekezwa ni maji au tende, hivyo unaweza kununua maji na ukampa tajiri akanywa cha awali baada ya magharibi kupigika na ukapata thawabu sawa na aliyefuturisha masikini.

" Hivyo wanaofuturisha matajiri, wenye uwezo hawapaswi kulaumiwa kwa sababu wanapata thawabu sawa na pengine walishafuturisha masikini kwa njia nyingine, tunachosisitiza ni vema masikini wakakumbukwa hususani wakati huu ambao pengine wana uhitaji mkubwa," amesema.

Amesema kutokana na wakati wa mfungo kuwa na ongezeko la mahitaji ikiwamo futari nzuri ni bora kuwakumbuka wenye uhitaji.

Chanzo: mwananchi.co.tz