Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheikh awataka Waislamu kuyaendeleza mema ya Ramadhan

61386 Pic+shein

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein ameongoza mamia ya Waislam katika swala ya Eid El Fitri huku wito ukitolewa kwa waumini wa dini hiyo kuendeleza mema kama ilivyokuwa wakati wa mfungo wa Ramadhan.

Swala hiyo imesaliwa katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja leo asubuhi Jumatano Juni 5, 2019 na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, siasa, dini pamoja na wananchi mbalimbali kutoka maeneo ya Zanzibar.

Akitoa nasaha katika Sala hiyo, Shekh Mohamed Ali kutoka ofisi ya Mufti amesema kukamilika kwa Ramadhan si mwanzo wa maasi kwa Waislam akiwasihi kuendelea na ibada kama ilivyokuwa kwa mwezi wa Ramadhan.

Amesema kufanya maasi baada ya saumu ni sawa na kujenga kisha ukabomoa, kitendo ambacho amesema hakuna hata mmoja anakifurahia.

Shekh Ali amewataka Waislam kuendeleza umoja wao kwa kushirikiana katika kusaidia hasa kwa wale wenye uwezo kuwaangalia zaidi wanyonge ili nao wawe na furaha katika kipindi hichi.

"Niwaombe sanaa ndugu zangu tuendelezae umoja wetu wa kudumisha amani na utulivu, tukiamini amani ndio chanzo halisi ya kufurahia kila jambo bila ya usumbufu au hofu," amesema.

Pia Soma

Miongoni mwa viongozi walioshiriki katika swala hiyo ni Makamu wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, Muftii wa Zanzibar, Saleh Omar Kaabi, Mama Mwanamwema Shein.

Pia, Spika wa Baraza la Wawakilishi,  Zuberi Ali Maulid, wawakilishi, wabunge, watendaji wa Serikali ya Zanzibar na Muungano pamoja na viongozi na wananchi wengine mbalimbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz