Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheikh Tabora aomba misingi bora kwa watoto

BAZAAA Sheikh wa mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: eatv.tv

Sheikh wa mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi, amesema upo umuhimu mkubwa wa kuwajengea watoto misingi imara ya dini itayowaongoza kuishi katika maadili mazuri na kuepukana na vitendo vya uhalifu wa kutumia nguvu na silaha ambavyo vimekuwa vikifanywa na vijana wadogo.

Sheikh Mavumbi ametoa kauli hiyo alipohudhuria mashindano ya Qu,rani ambayo yameandaliwa na taasisi ya kiislamu ya  Al  tijarah al rabiha charitable foundation kupitia chuo chake ya Maahad Oman Islamic  kilichopo eneo la  Ibologero, wilayani Igunga mkoani Tabora .

Amesema kwa sasa  kumekuwa na anguko kubwa la maadili kwa watoto hatua ambayo imekuwa ikisababisha wengi kujiingiza katika  matukio ya uhalifu.

Chanzo: eatv.tv