Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheikh Mkuu atoa msimamo ndoa kwa mtoto wa kike

82237 Pic+waislam Sheikh Mkuu atoa msimamo ndoa kwa mtoto wa kike

Wed, 30 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amesema kwa dini ya Kiislamu, mtoto wa kike akivunja ungo, anaruhusiwa kuolewa ikiwa atahitajika kufanya hivyo.

Alisema kwa maslahi ya elimu, mtoto huyo atapaswa kusubiri mpaka umri wa miaka 18 na kuendelea.

Mufti Zubeir alisema hayo juzi baada ya kuulizwa alivyopokea uamuzi wa Mahakama ya Rufani kukubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu ya kubatilisha vifungu vya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 vinavyoruhusu mtoto wa umri chini ya miaka 18 kuolewa.

SOMA ZAIDI: Mahakama ya Tanzania yahitimisha mjadala umri wa kuolewa

Shauri hilo lilifunguliwa na Rebecca Gyumi aliyejenga hoja kuwa vifungu hivyo vya sheria vinakiuka Katiba na kumnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata elimu.

Jana, Mufti, ambaye alihudhuria kongamano maalum la viongozi wa dini kuelekea uchaguzi lililoandaliwa na Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam, alisema hawana matatizo na mtoto wa kike anayeendelea na masomo. “Sisi watu wa dini tuna maneno yetu tunazungumza; ikiwa mtoto anaendelea na masomo na katika kuendelea kwake na masomo atalazimika asome, (basi) amalize masomo, kwa maslahi ya elimu,” alisema.

“Lakini ikiwa hakuna jambo lolote, huwezi kumuacha akae tu mpaka afikishe miaka 18 afanye ufisadi, ikifikia suala la namna hiyo apate mume aolewe tu, sheria ya kiislamu mtoto akibalehe anatakiwa aolewe endapo litatokea suala la kuolewa.”

Alisema ataolewa akiwa na umri wa miaka 18 na kuendelea ikiwa atakuwa kwenye masomo tu.

“Kwa maana ya kupata elimu inayomjenga mtoto si vibaya kufika miaka 18 na kuendelea,” alisema.

Kauli hiyo ni ya kwanza ya kiongozi wa juu wa dini hiyo tangu Mahakama ya Rufani ilipotoa hukumu yake ya kukubaliana na uamuzi wa mahakama ya chini kuhusu ndoa za utotoni.

Bado Serikali, ambayo sasa inatakiwa kufanya mabadiliko katika sheria hiyo ndani ya mwaka mmoja, haijatoa msimamo wake baada ya rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kugonga mwamba.

Awali, viongozi waliozungumzia suala hilo kwa nyakati tofauti walikuwa na maoni tofauti, huku Profesa Palamagamba Kabudi akionyesha jinsi lilivyo na ukakasi kutokana na imani, mila, desturi na tamaduni tofauti.

Akizungumza katika kongamano hilo, Askofu Mkuu Kanisa la Anglikana, Jimbo la Dar es Salaam, Jackson Sosthenes alisema uongozi imara si utaalamu wa kutoa hotuba au kupendwa na watu ila ni kuonyesha matokeo aliyotarajiwa.

Alisema umaskini na unyonge uliolifunika bara la Afrika si ukosefu wa rasilimali isipokuwa matokeo ya kukosekana kwa uongozi bora.

Kiongozi huyo alisema sifa za kiongozi bora ni uadilifu, kujali watu anaowaongoza, kutanguliza mbele maslahi yao, uwajibikaji na kufanyia kazi anayozungumza ikiwamo vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

SOMA ZAIDI: Mahakama ya Tanzania yahitimisha mjadala umri wa kuolewa

“Kiongozi bora lazima akubali kulaumiwa lakini asilaumike, awe jasiri na asiogope kufanya maamuzi. Tanzania ya viwanda inahitaji viongozi jasiri,” alisema Askofu Sosthenes.

“Yapo baadhi ya matatizo hapa nchini yanatokana na baadhi ya viongozi waliopewa dhamana kutowajibika ipasavyo jambo linalomfanya Rais Magufuli (John) kufanya mabadiliko ya mara kwa mara.”

Askofu Sosthenes alisema kiongozi bora anapaswa kugeuka nyuma na kuangalia kama watu anaowaongoza wanamfuata

“Wengi tunafahamu kuwa kiongozi ni mwonyesha njia, ni vizuri ifahamike kuwa yeye ni mwonyesha njia.

SOMA ZAIDI: Mahakama ya Tanzania yahitimisha mjadala umri wa kuolewa

Chanzo: mwananchi.co.tz