Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shehe wa Mkoa Singida afariki, kuzikwa leo

E62ac95fbcd33ccead51fbe680cb9bf8 Shehe wa Mkoa Singida afariki, kuzikwa leo

Fri, 16 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHEHE wa Mkoa wa Singida, Salum Mahami anatarajiwa kuzikwa leo mkoani humo.

Shehe Mahami alifariki dunia usiku wa kuamkia jana wakati akipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dar es Salaam.

Mahami aliyeteuliwa na Baraza la Ulamaa katika kikao chake cha Aprili 4, mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir kuwa shehe wa mkoa huo.

Mufti Zubeir jana alitoa taarifa ya msiba kupitia taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari cha Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma alilieleza gazeti hili kuwa mwili wa marehemu ulitarajiwa kusafirishwa jana hadi Singida kwa ajili ya maziko leo.

“Ni kweli kiongozi huyo amefariki na kwa sasa taratibu zinafanywa ili baadaye jioni ya leo (jana) mwili wake uweze kusafirishwa hadi mkoani Singida kwa ajili ya mazishi. Bakwata imepokea msiba huo kwa majonzi makubwa na tunamuombea kwa Mungu akapate kupumzishwa salama,” alisema Mruma.

Alisema Shehe Mahami alikuwa kiongozi mwadilifu, mchapa kazi na msikivu kwa kila mtu huku michango yake mbali mbali ndani ya Bakwata ikisaidia kuhakikisha maendeleo ya chombo hicho kikubwa cha Waislamu nchini yanasonga mbele kwa kasi.

Aidha, mbali na kuitumikia nafasi hiyo ya Shehe wa Mkoa, Mahami pia aliwahi kuitumikia siasa akiwa Diwani wa Kata ya Majengo na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa vipindi kadhaa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz