Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shehe ataka waumini kuzingatia maadili ya Uislamu

Bf510d881a7d594cdc3490ffdf47943d.png Shehe ataka waumini kuzingatia maadili ya Uislamu

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHEHE wa Mkoa wa Geita, Alhaji Yusuph Kamoga, ametoa mwito kwa waumini wa dini ya Kiisalmu mkoani hapa kuacha visingizio na vinyongo kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, badala yake wazingatie maadili ya Uislamu na kutimiza wajibu wa kufunga mwezi mzima kama inavyoelekezwa.

Alitoa mwito huo juzi ofisini kwake wakati akizungumuza na waandishi wa habari kuelezea maandalizi ya Waislamu mkoani hapa kuelekea Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani ulioanza jana.

Alisema Waislamu wanapaswa kufuata mafundisho ya dini yao kwa kila mmoja kufunga katika kipindi hiki isipokuwa wenye sababu muhimu.

"Tunawahimiza Waislamu kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao kwetu Waislamu, tunaamini kabisa ni mwezi wenye utukufu na baraka nyingi kwa anayeutekeleza katika mafundisho ya Uislamu,” alisema.

"Nawaomba Waislamu kuyatekeleza vyema yaliyo ndani ya Mwezi wa Ramadhani kama wajibu kwao, kwa kuwa Mungu ametuagiza kufanya kwa maana tunafunga na kuwa na matendo mema ndani ya mwezi mtukufu na kuendelea,” alisema.

Akaongeza: "Wajiepusha na maovu kwani kufunga ni ibada ambayo ukikiuka maadili yake, inaharibika; kwa hiyo lazima kuzingatia ibada kwa hiyo Mwenyezi Mungu ili aipokee, lakini ukifunga ndani yake ukaweka vitu ambavyo havifurahishi funga yako haitokubalika," alisema Shehe Alhaji Yusuph.

Shehe wa Kata ya Kalangalala wilayani Geita, Tuwa Mohamed, aliwaomba vijana kuutumia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama mwanzo wa kuacha matendo maouvu yasiyomfurahisha Mungu ukiwamo, uzinzi na uasherati.

Naye Shehe Mbaraka Bin Abdul Bary aliwaomba wazazi na walezi kuhakikisha familia zao zinatimiza yanayotakiwa kufanyika katika kipindi ncha mfungo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz