Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawapongeza wananchi, kanisa katokili Mbulu

11516 MBULU+PIC TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbulu. Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewapongeza wananchi wa wilaya za Babati na Hanang mkoani Manyara na Karatu mkoani Arusha kwa kupata askofu wa tano wa jimbo la Mbulu.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Agosti 12, 2018 katika misa takatifu ya kumweka wakfu Askofu Anthony Lagwen.

Profesa Kabudi aliyemuwakilisha Rais John Magufuli, amesema Kanisa Katoliki limekuwa msaada mkubwa kwa Serikali kwa kutoa huduma ya elimu, afya na maji hasa kwa watu wa kawaida.

Amesema jimbo la Mbulu lililoundwa tangu mwaka 1953 limekuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha jamii ya eneo hilo inapata huduma za kiroho na kimwili.

"Tunapongeza kanisa katoliki jimbo la Mbulu kwa kutoa huduma za afya ikiwemo hospitali za misheni za Dareda na Bashnet wilayani Babati," alisema.

Amepongeza jimbo hilo kumiliki kituo cha redio Habari Njema ambacho kwa namna moja au nyingine kinatoa huduma ya uinjilishaji na kuhabarisha jamii.

"Kituo hicho cha redio kiendelee kusisitiza amani kwani bila uwepo wa amani hakutawezekana kufanyika chochote," amesema.

Amesema taasisi za dini kwa kiasi kikubwa zimechangia maendeleo mengi na ustawi wa jamii hivyo serikali itaendelea kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha jamii inasonga mbele.

Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, mwadhama Policarp Kardinali Pengo amesema japokuwa Askofu Lagweni ni mzaliwa wa jimbo la Mbulu lakini atakumbana na changamoto zile zile wanazokumbana nazo maaskofu wanaoongoza majimbo ambayo hawajazaliwa.

"Mimi siwezi kuona Sumbawanga ndiyo bora zaidi kuliko sehemu ninayoongoza waumini hivyo nawe waongoze waamini kama inavyopaswa kuwaongoza," alisema Kardinali Pengo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz