Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaombwa kutunga sheria kali kuwabana wanaotupa watoto

Fri, 12 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Serikali imeombwa kutunga sheria kali, ambayo itadhibiti matukio ya kutupwa watoto wachanga na wazazi wao kwa kisingizio cha hali ngumu ya maisha.

Mkuu wa kituo cha kulea watoto yatima cha Grace Orphanage and Childred Center kilichopo Kata ya Baraa jijini Arusha, Anna Kivuyo alitoa wito huo leo Oktoba 10, 2018 wakati akipokea msaada wa watoto wa kituo hicho kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika la Posta Arusha.

Amesema hivi sasa kutokana na kukosekana sheria kali, kumekuwepo ongezeko la watu kutupa watoto wao wachanga ama ndugu walioachiwa watoto na wazazi wao.

“Wazazi wanaotelekeza watoto ni sawa na wauaji, wanawatupa watoto sehemu ambazo wanaweza kufariki kutokana na hali ya hewa ama kuliwa na wanyama,” amesema.

Meneja wa Shirika la Posta Arusha na Manyara, Dongwe James amesema bila kuwepo sheria kali ni vigumu kudhibiti tatizo la watoto kutupwa.

“Kwa kutambua umuhimu wa watoto kuishi kwa furaha baada ya kutelekezwa sisi wafanyakazi wa posta tumeona tujitolee msaada wa vyakula, vinywaji, sabuni na sukari,” amesema.

Hilda Malisa amesema wanaotupa watoto wengi ni wasichana ambao wanakata tamaa ya maisha kutokana na kutelekezwa na waume zao ama kupata mimba.

Kituo cha watoto yatima cha Grace kilianzishwa mwaka 2016 na kina watoto 10 wakiwemo wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

Chanzo: mwananchi.co.tz