Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SERIKALI KUENDELEA KUTOZA KODI TAASISI ZA DINI

1cb43a76029775445449630e9382265b.jpeg SERIKALI KUENDELEA KUTOZA KODI TAASISI ZA DINI

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inalazimika kuzitoza kodi taasisi za kidini zinazotoa huduma za afya na elimu, kwa sababu baadhi ya taasisi hizo zina mazingira ya kuonekana kufanya kazi kibiashara na sio kihuduma.

Amesema endapo serikali itaondoa kodi kwa taasisi za kidini, ambazo utendaji wake unaendana na taasisi binafsi, kutakuwa hakuna uwanja sawa wa kufanya shughuli hizo kwani sekta binafsi watashindwa kuhimili.

Rais Samia amesema hayo leo (Julai 8, 2021) wakati akishiriki Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) mkoani Morogoro.

Aidha, amesema kuwa serikali imejipanga kuangalia mfumo mzima wa kodi wa nchini, ili kuona zipi za kufuta, kuzipunguza au kuzisamehe na kuwa tayari serikali imeanza kufanya mapitio ya kodi na kufuta baadhi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz