Rombo. Ulevi uliopindukia hasa kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea wa kujihusisha na unywaji pombe haramu ya gongo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro umekua ni chukizo kwa jamii na baadhi ya viongozi wa dini.
Kutokana na hali hiyo, viongozi wa Kanisa Katoliki Rombo wameendelea kupigilia msumari watengenezaji wa pombe hizo wakisema endapo hawataacha kutengeneza watatengwa na kanisa pamoja na waumini wa dini hiyo kwani pombe hizo zinaharibu nguvu kazi ya vijana wengi
Kauli ya kutengwa kwa watengenezaji gongo imesemwa juzi Alhamisi Juni 27, 2019 na Mkuu wa vikarieti ya Vunjo, Padre Valerian Msafiri wakati wa adhimisho la misa Takatifu ya Jubilee ya miaka 50 ya Halmashauri ya Walei iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji.
“Leo tunasherekea sikukuu ya kuzaliwa kwake Yohana Mbatizaji, alijitenga na maovu, alikataa dhambi, nyie mnafanya nini kwa nini msiwatenge hao watengenezaji gongo? mnasubiri nini watengeni, mkifanya hivyo mtafanana na Yohane Mbatizaji na wilaya yenu itakua na Mwanga,” alisema Padre Msafiri.
Awali, akisoma taarifa ya Parokia hiyo, Katibu wa Parokia, Eleuter Massawe amesema changamoto kubwa katika wilaya hiyo ni ulevi uliopindukia hasa vijana ambapo wengi wao wamekua wakinywa gongo hali ambayo inawafanya washindwe kufanya kazi ya kuzalisha.
“Changamoto kubwa iliyopo katika wilaya yetu ni kukithiri kwa unywaji wa gongo hasa kwa vijana, wengi wao wamekua wakinywa pombe haramu ya gongo na pombe nyingine ambazo hazina viwango jambo ambalo linawaangamiza vijana wengi,” alisema Massawe.
Pia Soma
- Naibu Waziri Kanyasu atoa agizo kwa TFS
- Mama na mwanaye wanyolewa kipara baada ya kukataa kubakwa
- Askofu Bagonza aingia katika Ubunge wa Lissu na maswali tata
“Kutengwa na kanisa ni adhabu kubwa sana katika dini yetu, hivyo uamuzi huo ukitekelezeka watu hawa huenda wakapunguza kutengeneza pombe hizo, kanisa linafanya vizuri sana ili kuokoa kizazi kijacho, maana vijana wetu wengi wameharibiwa na pombe hata kufanya kazi za kuzalisha hawawezi tena,” alisema Tesha.