Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi Sheikh Walid awa Sheikh Mkuu wa Dar

Sheikh Walid Alhad Rasmi Sheikh Walid awa Sheikh Mkuu wa Dar

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe wa Baraza la Maulamaa, Sheikh Hamid Jongo amemtangaza Sheikh Walid Alhad Omar Kawambwa kuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Sheikh Walid ameteuliwa jana Desemba 17, 2023 katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) yaliyofanyika Makao Makuu ya Bakwata Kinondoni Jijini hapa.

Kabla ya Uteuzi huu Sheikh Walid ambaye ni Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kichangani, Magomeni alikuwa anakaimu nafasi hiyo, iliyokua inaongozwa na aliekua Shekhe wa Mkoa huo Sheikh Alhad Mussa Salum, ambae Baraza la Ulamaa lilitengua uteuzi wake Februari 2, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live