Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais TEC atuliza waumini vifo maaskofu wa Katoliki

58251 Pic+TEC

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC), Mhashamu Gervas Nyaisonga amewataka waamini kupokea msiba uliolikumba Kanisa Katoliki baada ya maaskofu wastaafu wawili kufariki dunia juzi na usiku wa kuamkia jana.

Maaskofu hao ni Gabriel Mmole aliyetumikia jimbo la Mtwara na ambaye alifariki Mei 15, na walitumikia majimbo ya Mtwara na Emmanuel Mapunda aliyetumikia jimbo la Mbinga.

Amesema huo ni msiba mkubwa na mzito, lakini waamini waupokee kwa kuwa mapenzi ya Mungu yametimizwa.

Nyaisonga, ambaye pia ni askofu wa Jimbo Kuu la Mbeya, alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na Mwananchi, huku akiwataka Wakatoliki na wananchi kwa ujumla nchini, kutoshtushwa na vifo vya maaskofu hao kwa sababu ni vifo vyema.

“Watu wasishtuke sana. Hawa waliofariki dunia ni maaskofu wetu waliotumikia na wana umri wa zaidi ya miaka 80,” alisema.

“Sasa unajua unapokuwa mzee mwili unakuwa dhaifu kiasi. Wasishtuke ni vifo vyema na vimewakuta katika uzee na ukiwa katika hatua hii, mwili unaweza ukapata shida.”

Pia Soma

Alisema vifo hivyo ni vya kusifiwa kwa sababu walishalitumikia kanisa hilo na walipofikisha miaka 75 walikabidhi vijiti kwa wenzao, lakini waliendelea kuishi vizuri na kushirikiana na waliowarithi.

Alisema Askofu Mmole aliongoza jimbo la Mtwara kwa miaka mingi, wakati Mapunda aliongoza Mtwara kwa zaidi ya miaka 25.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa TEC, Padri Charles Kitime maziko ya Askofu Mmole (80) yatafanyika Mei 21, mkoani Mtwara, wakati Askofu Mapunda (84) atazikwa Mei 24 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Chanzo: mwananchi.co.tz