Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia apewa mwaliko na Papa Francis Vatican

Samia X Rugambwa.jpeg Rais samia na Cardinali Rugambwa

Sun, 21 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajia pia kufanya Ziara ya Kitaifa Vatican kuanzia tarehe 11 - 12 Februari, 2024 kufuatia mwaliko wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba leo Januari 21, 202224 inaeleza lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano wa uwili (bilateral cooperation) kati ya Tanzania na Vatican ambapo atakutana kwa mazungumzo na Baba Mtakatifu Francis pamoja na Katibu wa Vatican Mhe. Pietro Parolin.

Uhusiano kati ya Tanzania na Vatican ulianza miaka ya 1960 wakati ambapo Vatican ilianzisha Ubalozi wake hapa nchini. Tangu wakati huo Vatican kupitia Kanisa Katoliki imekuwa mstari wa mbele katika kujishughulisha na masuala ya kiroho, amani, elimu na program za afya hapa nchini.

Vatican kupitia Kanisa Katoliki imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya elimu kabla na baada ya uhuru wa Tanzania Bara kwa kutoa elimu kwa Watanzania wa dini zote. Kanisa Katoliki linakadiriwa kumiliki zaidi ya shule za chekechea 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 245, vyuo vya ufundi 110, na vyuo vikuu 5.

Katika Sekta ya Afya, Vatican kupitia Kanisa Katoliki imeendelea kutoa huduma bora za afya kwa Watanzania ambapo inakadiriwa hadi sasa kanisa linaendesha takriban taasisi 473 za afya. Taasisi hizi zimechangia kuzalisha wataalam wa afya nchini. Pia mchango wa kanisa kwenye sekta ya afya umesaidia kuimarisha afya za watu na kupunguza vifo.

Itakumbukwa kuwa, mwaka 2016 Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania alimwalika Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, yaani Baba Mtakatifu Francis kutembelea Tanzania.

Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya ziara hiyo haikuwezekana na badala yake kwa wakati huu, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekubali mwaliko wa kiongozi huyo na kufanya ziara Vatican.

Akiwa Vatican, Mheshimiwa Rais atakutana kwa mazungumzo na Baba Mtakatifu Francis pamoja na Katibu wa Vatican, Mhe. Pietro Parolin.

Uhusiano kati ya Tanzania na Vatican ulianza miaka ya 1960 wakati ambapo Vatican ilianzisha Ubalozi wake hapa nchini. Tangu wakati huo Vatican kupitia Kanisa Katoliki imekuwa mstari wa mbele katika kujishughulisha na masuala ya kiroho, amani, elimu na program za afya hapa nchini.

Vatican kupitia Kanisa Katoliki imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya elimu kabla na baada ya uhuru wa Tanzania Bara kwa kutoa elimu kwa Watanzania wa dini zote. Kanisa Katoliki linakadiriwa kumiliki zaidi ya shule za chekechea 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 245, vyuo vya ufundi 110, na vyuo vikuu 5. 

Kupitia shule na vyuo hivi Kanisa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania limechangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha viongozi na wataalam mahiri kwenye maeneo mbalimbali.

Katika Sekta ya Afya, Vatican kupitia Kanisa Katoliki imeendelea kutoa huduma bora za afya kwa Watanzania ambapo inakadiriwa hadi sasa kanisa linaendesha takriban taasisi 473 za afya. Taasisi hizi zimechangia kuzalisha wataalam wa afya nchini. Pia mchango wa kanisa kwenye sekta ya afya umesaidia kuimarisha afya za watu na kupunguza vifo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live