Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Mwinyi kushirikiana na JUMAZA kukuza dini

4acfcdb7efde92cba055ef88d9217e7a Rais Mwinyi kushirikiana na JUMAZA kukuza dini

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameihakikishia Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) kuwa serikali itashirikiana vyema na jumuiya hiyo kwenye kujenga misingi ya dini ya kiislamu visiwani humo.

Dk Mwinyi amesema hayo alipofanya mazungumzo na viongozi wa jumuiya hiyo wakiongozwa na Kaimu Katibu wao, Sheikh Ali Abdalla Amour Ikulu ya Zanzibar.

“Nasema wazi miongoni mwa mambo makubwa yanayopaswa kupewa kipaumbele katika kujenga misingi ya dini ya Kiislamu ni umoja, amani na mshikamano” amesema Dk Mwinyi.

Chanzo: habarileo.co.tz