Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Mwinyi: Taasisi za Dini zina mchango kuendelea amani

328691586 881504616512614 4343117130834996044 N 1140x640 Dkt. Hussien Ali Mwinyi

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussien Ali Mwinyi amesema Taasisi za dini nchini zina mchango mkubwa kwa Serikalini ili kufanikisha kuendeleza amani.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Jumuiya Sunni Jamaat, walipofika ofisini kwake hii leo Februari 2, 2023 kujitambulisha.

Amesema, taasisi hizo zinawalea vijana kiimani, kiweledi, kiujasiri na kiuzalendo kwa manufaa ya Taifa na viongozi wao, jambo ambalo linaimarisha amani na uthubutu wa kuyafikia maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live