Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC mpya Morogoro awaonya wafugaji, watumishi wa umma

77071 RC+PIC

Wed, 25 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Mkuu mpya wa Mkoa wa Morogoro (RC), Loatha Sanare amesema kuteuliwa kwake kuwa mkuu wa mkoa huo wafugaji wa Kimasai wasione ni fursa kwao kuwatetea bali yeye ameteuliwa kuongoza makabila yote.

“Mimi sio mkuu wa mkoa wa Masai tu mimi ni mkuu wa mkoa wa makabila yote, nitafanya kazi kwa kufuata misingi na sheria zilizopo na si vinginevyo, sitaki kuona migogoro ya wakulima na wafugaji inaleta aibu katika mkoa wetu,” alisema.

Sanare alisema hayo jana Jumatatu Septemba 23, 2019 wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa juu wa serikali ya mkoa ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, wakuu wa  wilaya, wakurugenzi wa halmashauri pamoja na wakuu wa taasisi za umma.

Katika kikao hicho, pia alikuwepo mtangulizi wake, Dk Stephen Kebwe aliyemkabidhi ofisi.

Alisema anajua lazima wafugaji hao wa Kimasai wafurahi kusikia mfugaji mwenzao kuteuliwa kwani ni ndugu yao na kwamba atachukua hatua pindi atakapobaini kuna ukiukwaji sheria za nchi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa, aliwataka watumishi wa Serikali kufanya kazi kwa weledi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea huku akiwataka wakuu wa wilaya kufungua milango yao na kusikiliza wananchi ili kuondoa malalamiko kutoka kwao na kuonyesha upendeleo kwa baadhi ya wananchi.

Pia Soma

Advertisement

Alisema ofisi ya mkuu wa mkoa itakuwa wazi wakati wote na kwamba yeye na katibu tawala mpya wa mkoa aliyeteuliwa Emanuel Kalobelo watahakikisha wanashirikiana na watendaji wa umma ambao wataonyesha kwenda na kasi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Akizungumza wakati wa akimkabidhi taarifa ya mkoa, Dk Kebwe alielezea kuwa kuondolewa kwake haoni kwamba ni masikitiko kwake bali ameongezewa wasifu na imekuwa historia katika maisha yake.

“Hata kesho na keshokutwa nikiondoka dunia nitaandikwa kuwa aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, hii imekuwa historia kwangu namshukuru sana mheshimiwa Rais kwa kuniteua na kuniongezea wasifu,” alisema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz