Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kukwa aeleza mwaka 2020 utakavyotumika kumlinda mtoto

90019 Mimba+pic RC Kukwa aeleza mwaka 2020 utakavyotumika kumlinda mtoto

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (RC) nchini Tanzania, Joachim Wangabo amesema mkoa huo umepanga mwaka 2020 kuwa mwaka maalumu kwa ajili kumlinda mtoto pamoja na kuhakikisha heshima yake inadumishwa.

Lengo ni kuhakikisha haki ya mtoto inapatikana, anathaminiwa, anapata elimu na  anakuwa na maendeleo na malezi ya kimwili na kiroho tangu akiwa mdogo ili aje kuwa na utu.

Wangabo aliyasema hayo jana Jumatano Desemba 25, 2019 alipokuwa akitoa salamu zake za Krismasi kwa wananchi  kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Tanganyika.

Katika ibada hiyo aliwataka wananchi wa mkoa kusherehekea sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya kwa kutafakari nafasi za watoto katika familia.

“Serikali imejipanga kuhakikisha mwaka 2020 unakuwa ni mwaka maalum wa mtoto katika mkoa wetu  kwa sababu kwa muda mrefu wananchi wameshindwa kuthamini maendeleo ya mtoto kiafya na kielimu.”

“Watoto wamekuwa wakienda shule bila ya kula chochote nyumbani na hata wakifika shuleni ambapo anakaa zaidi ya saa kumi hapewi chakula chochote hali inayopelekea watoto hao kushindwa kuzingatia masomo,” amesema Wangabo.

Aliwasisitiza wananchi hao kuwapa watoto haki zao ikiwamo chakula ili na kuacha  manyanyaso ya kuwatukana na kuwapiga ovyo, kuwachoma moto, kuwabaka.

Alisema Sheria ya Mtoto Na 21 ya mwaka 2009 inaelekeza utoaji wa huduma za ulinzi na ustawi wa mtoto.

Aidha sheria imetoa wajibu kwa watoto kuwasaidia wazazi wao kazi zisizo hatarishi na ambazo hazina madhara kiafya na zitakazompa mtoto fursa ya kushiriki katika masomo na michezo.

“Vilevile jamii ina wajibu wa kuhakikisha watoto wanaishi katika maadili mema na kutoa taarifa kwa mamlaka za serikali iwapo mtoto ataonekana kuzurura na haendi shule au anajishughulisha na ajira hatarishi,” aliongeza.

Chanzo: mwananchi.co.tz