Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Ndalichako apongeza ujenzi shule ya sekondari Bwiru

68014 Pic+ndalichako

Wed, 24 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Kiasi cha Sh974 milioni kimetumika katika ujenzi na ukarabati wa Shule ya Sekondari ya wasichana Bwiru jijini Mwanza.

Mradi wa ujenzi huo uliofadhiliwa na Taasisi ya Elimu (TEA) umeanza Februari 2018 na kukamilika Septemba 2018.

Akizungumza leo Jumatano Julai 24, 2019 wakati akikagua  maendeleo ya mradi huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema amefurahi jinsi fedha zilizotengwa zilivyotumika hadi nyingine kubaki.

Amepongeza chuo cha Sayansi na Tekinolojia cha Mbeya (Must) kwa usimamizi mzuri na kazi imeonekana.

Awali Mkuu wa shule hiyo, Mekitilda Shija amesema pamoja na faida nyingine, mradi wa ukarabati umeboresha mazingira ya shule ikiwemo ujenzi wa bweni, uzio na jengo la utawala ambavyo vyote vilikuwa ni changamoto.

Amesema shule ina wanafunzi 812, kati yao 390 kidato cha tano na 422 wakiwa kidato cha sita.

Pia Soma

"Huenda idadi hiyo ikaongezeka maana kidato cha tano bado waendelea kuja kwa sababu lengo letu ni kuwasajili wanafunzi 447," amesema Mekitilda

Waziri Ndalichako aliipongeza shule hiyo kutopata daraja sifuri katika matokeo yake, "Mnafanya vizuri maana mwaka jana 2018 mlikuwa nafasi ya 17 kati ya 29 na mwaka 2019 mmesogea hadi nafasi ya 9 kimkoa."

Chanzo: mwananchi.co.tz