Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pasta aungana na waumini kuomba mvua ikome

Pasta Aungana (1) Pasta aungana na waumini kuomba mvua ikome

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Video moja ya mchungaji akiungana na waumini wake kuombea mvua kunyeshewe wakati wa kongamano la mahubiri kwenye sehemu tambarare imevutia maoni mengi kinzani katika mitandao ya kijamii.

Kutokana na video hiyo, mchungaji huyo alikuwa anaongoza mahubiri kwenye kiwanja tambarare ambapo walikuwa wamekita hema na maturubai wakati mbingu zilikasirika na kupwa.

Mtumishi wa Mungu aliamua kuonesha nguvu zake za kipekee na za upako kwa kuisitisha mvua kukoma kunyesha ili kutoa nafasi kwa neno la Mungu kuendelea kutaradadi.

Hapo ndipo alianza kufanya maombi huku akiongea kwa lugha za ndimi na ghafla waumini wake wengi waliungana naye na kundi hilo kubwa la watu likajikita katika kufanya maombi ya kuifukuza mvua.

Wengine walionekana wakinyeshewa huku wakiruka kwenye mvua kwa maombi ambayo hata hivyo hayakuonekana kuwa na athari yoyote chanya kwa mvua kwani iliendelea kutiririka kwa kishindo cha awali.

Video hiyo imevutia maoni mengi kutoka kwa watu, baadhi wakisema kwamba dini zimefikia hatua ya kuchukulia poa akili za watu na kuwavurukuta kabisa kutoka kwa kufikiria kufanya kilicho sahihi kutokana na nadhiri za bongo zao.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu kwenye chapisho hilo Instagram; “Hapana, huwezi kumjaribu Mungu. Mwezi uliowekwa kwa mazishi , Hali ya hewa chochote kinaweza kutokea, kwa kunyesha,” Papi Dickie alisema.

“Hii mvua kawaida haitonyesha kwa muda mrefu, hata wao wanajua hilo na itakapoisha kunyesha watakwenda na kujipiga vifua kwamba ni wao wamefanya muujiza wa kusimamisha mvua,” Official Capello alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live