Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paroko: Msikufuru, muwe na matumaini

Ffb8a7d4125471af6321f75ec5e4024e Paroko: Msikufuru, muwe na matumaini

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

PAROKO wa Parokia ya St Peter Oysterbay Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Alister Makubi amewataka Watanzania wasisikitike na kufikia hatua ya kukufuru bali wawe na matumaini, wamshukuru Mungu aliyemjalia maisha Rais John Magufuli.

Padri Makubi alisema Rais Magufuli alifanya mambo mengi mazuri kwa haraka kabla ya kifo chake hivyo kila mmoja anapaswa kufanya mambo aliyokabidhiwa na Mwenyezi Mungu vizuri na kwa haraka bila kupoteza muda kama alivyofanya.

Alisema hayo jana wakati akiongoza Ibada ya kumwombea Rais Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, mwaka huu.

Rais Magufuli alikuwa muumini Mkatoliki wa parokia hiyo ya St Peter na alishiriki mara nyingi ibada za misa za Jumapili kanisani hapo.

“Tupo katika mioyo mizito na kipindi kigumu kwa kuondokewa na Rais wetu John Magufuli, tupo katika kipindi cha Kwaresma tunaelekea Juma Kuu, kuna mateso, kifo na ufufuko mambo ambayo Bwana wetu Yesu Kristo alitufundisha, haya tunayokumbana nayo yatapita, hakuna hata mmoja atakayebaki hapa milele, sisi sote hapa tuko hija, tupo safarini, makao yetu sisi siyo hapa, makao yetu ni kule Mbinguni ambako Mungu yupo,” alisema Padri Makubi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Martha Qorro ambaye alikuwa anasali Jumuiya ya Mtakatifu Mariagoreth pamoja alisema Dk Magufuli alikuwa hakosi sala za jumuiya na alishiriki michango yote ya kanisa.

Sista Jastina Mahemba wa Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge, alisema Rais Magufuli alikuwa kama baba na mlezi wa watu wote kwa kuwa hakuwabagua Watanzania kwa misingi ya dini, ukabila, rangi au siasa

Chanzo: www.habarileo.co.tz