Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa kutembelea nchi za Uarabuni

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Vatican. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis anaanza ziara katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Katika ziara yake ya siku tatu, Papa Francis atahutubia kwenye mkutano unaowaleta pamoja viongozi wa dini mbalimbali na atakutana na Sheikh Ahmed al Tayeb, Imam wa Al Azhar, taasisi ya elimu ya Kiislamu ya Cairo.

Kabla ya kumaliza ziara hiyo ataongoza misa kubwa mjini Abu Dhabi ambapo waumini wapatao 130,000 wanatarajiwa kuhudhuria.

Ziara hiyo ya papa inaonekana kama msingi mkuu wa kuwa na mdahalo wa dini mbalimbali katika kanda hiyo.

Umoja wa Falme za Kiarabu unajivunia hadhi ya kuheshimu uwepo wa dini nyingine na tamaduni mbalimbali.

Mrithi wa kiti cha ufalme wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mohammed bin Zayed al Nahyan ambaye amemualika Papa nchini mwake, amemtaja Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kuwa mtu wa amani na upendo.



Chanzo: mwananchi.co.tz