Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Papa hatoenda Uganda kukutana na maaskofu

43230 Pic+papa Papa hatoenda Uganda kukutana na maaskofu

Mon, 25 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala. Kongamano la Maaskofu limetangaza kuwa kiongozi wa Kaniasa Katoliki duniani, Papa Francis hatahudhuria kongamano la maaskofu wa Afrika ambalo limepangwa kufanyika Julai, 2019 kama alivyoalikwa.

Katibu wa Baraza la Maaskofu Uganda, John Baptist Kauta amesema wamepokea waraka kutoka ofisi ya Rais ukisema kiongozi huyo hatahudhuria kongamano hilo litakalowajumuisha maaskofu 400 wa Afrika na Madagascar.

Baraza la Maaskofu nchini Uganda lilimwomba Rais Yoweri Museveni kumwalika kiongozi huyo wa kiroho ambaye pia ni mkuu wa mamlaka ya Vatican.

Jumuiya ya baraza la maaskofu wa Afrika na Madagascar (Cecam) ilizinduliwa na Papa Paul VI Julai, 1969 nchini Uganda na ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Papa kuzuru Afrika.

Kongamano hilo mwaka huu linaadhimisha mwaka wake wa 50 tangu lianzishwe na linatumika kama jukwaa kwa maaskofu kutoa maoni yao na kuzungumza kwa sauti moja kuhusu masuala yanayohusu kanisa Katoliki.

Maandalizi ya kuadhimisha Jubilii ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo yalianza tangu mwaka jana na kilele chake kitakuwa Julai mwaka huu.

Waandaaji walitumaini Papa Francis aliyezuru Uganda mara ya mwisho Novemba, 2015 angehudhuria sherehe hizo.



Chanzo: mwananchi.co.tz